0


Guardiola
MANCHESTER, ENGLAND
LOUIS VAN GAAL amekunua meno yake, kisha akaachia kicheko na kumpiga kijembe kocha mtarajiwa wa Manchester City, Pep Guardiola kwamba imekula kwake kwani timu atakayorithi msimu ujao haitakuwamo kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya.

City wakiwa wamelowa.
Van Gaal amesema baada ya kuichapa Man City 1-0 Jumapili na hivyo kubakiza pointi moja tu kuingia kwenye nne bora, Mdachi huyo anaamini kikosi chake cha Man United ndicho kitakachomaliza ligi kwenye nafasi hizo nne za juu na kuipiga kikumbo Man City.
Man City inayoshika nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi, inaizidi Man United kwa pointi moja tu na Van Gaal anasisitiza nafasi sasa ni yao kuwaondoa mahasimu wao katika nafasi hiyo na kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.

Rashford akifanya yake
Van Gaal alisema timu tatu za juu kwenye msimamo bado zipo mbali kuzifikia kwa pointi, lakini kwa kuanza kitu rahisi ni kuiondoa Man City kwenye nafasi ya nne kuwa kuwa wapo juu kwa pointi moja tu.
Van Gaal alisema: “Sasa la kila kitu kipo kwenye mikono yetu. Tunachopaswa ni kushinda tu mechi zetu. Tuna mechi nyingi nyumbani kuliko ugenini na ni  wazi tumekuwa hatupotezi sana tunapokuwa Old Trafford.

Pellegrini asijue la kufanya
“Niliona hali ilivyokuwa vyumbani baada ya mechi, kulikuwa na furaha kubwa. Nadhani hili litachangia kuamsha molari.”
Kumekuwa na wasiwsi kwamba huenda Guardiola akarithi kikosi cha Man City ambacho hakitakuwamo kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao baada ya nafasi ya kumaliza kwenye nafasi nne za juu kuwa ngumu upande wao kwa siku za karibuni.

Van Gaal akifurahia jambo
Bao la kipindi cha kwanza la Marcus Rashford lilitosha kuizamisha Manchester City na kumfanya kocha Manuel Pellegrini kukwepa kuzungumza na vyombo vya habari baada ya kipigo hicho.

Post a Comment

 
Top