MADRID, HISPANIA
CRISTIANO RONALDO anataka mama yake
apewe ulinzi maalumu wa kumlinda muda wote lakini mama huyo hataki. Dolores Aveiro, 61, amesema nyota huyo wa zamani wa Manchester United ana hofu kuwa mama yake anaweza kuwindwa kama hatakuwa na usalama wa kutosha.
Mama huyo wa watoto wanne alisema kwenye mahojiano: “Ninapokwenda sehemu yoyote, Ronaldo husema: ‘Mama anatakiwa apewe ulinzi,’ lakini kamwe sitaki.
“Najisikia furaha na nadhani sihitaji mlinzi (body guard). Naishi kwa amani sana.
... Ronaldo na mama yake.
“Ninakuwa na wasiwasi zaidi
ninapokuwa na Cristiano lakini kamwe sijawahi kusumbuliwa.”Dolores, ambaye alinusurika na ugonjwa wa kansa ya matiti baada ya kugunduliwa mwaka 2007, pia alidai anajisikia sasa vizuri kuliko siku za nyuma.
Alimwambia Mtangazaji wa TV ya Ureno na Mwandishi Julia Pinheiro: “Ninavaa kile ninachokitaka na sina hofu watu wanasema nini juu yangu. Ninajisikia vizuri kama nina miaka 30.”
Mama wa Ronaldo akipika , nyumbani, Madrid
Dolores amekuwa akikwepa kuonekana
machoni mwa watu mpaka miaka ya hivi karibuni alipojiunga na Mtandao wa Twitter Novemba mwaka
jana baada ya kufungua Akaunti ya Instagram. Kwa kawaida amekuwa ‘akitwiti picha zake akiwa na ndugu wakiwemo madada wawili wa Ronaldo, Elma na Katia pamoja mtoto wa staa huyo Cristianinho.
Katika kuhakiki wafisu wake uliotolewa Julai 2014, aliweka wazi kwamba yeye ndiye aliyemchukua Cristianinho kutoka katika hospitali binafsi ya Florida Julai 2010, kuzua minong’ono kwamba mtoto huyo amezaliwa na mama ambaye aliyekodiwa.
Ronaldo na mama yake
Mama huyo aliuzua kishindo pale
alipokiri katika kitabu kwamba alishindwa kuitoa mimba ya Ronaldo, alikuwa akinywa
bia za moto na kukimbia sana mpaka alipomzaa baada ya daktari kukataa kumsadia
kutoa mimba yake ya nne.
...Ronaldo
Mama huyo wa watoto wanne ambaye aliolewa
na mume mlevi, Dinis aliyekufa kwa maradhi ya ini Septemba 2005, anautimia muda
wake mwingi kuwa karibu na mwanaye katika nyumba za watu mashuhuri (VIP)
zilizopo Madrid ambako Gareth Bale pia ana nyumba akisadia kumlea mjukuu wake, ambaye
pia anajulikana kama Cristiano Jr.
...akiwa kazini
Juni mwaka jana aliripotiwa
kusimamishwa Uwanja wa Ndege wa Madrid na kulazimishwa kukabidhi Pauni 35,000
ambazo zilionwa na mlinzi katika begi lake. Taarifa zinasema mama huyo alikuwa na kiasi cha pesa ambacho hakukitolea maelezo.
Kosa hilo lilichukuliwa kama ‘kosa la kiutawala’ badala ya kosa la kihalifu. Chanzo cha karibu na mama huyo kimesema iliaminika hali hiyo ilitokana na ujinga wake wa kisheria wa kujua mipaka ya kifedha kuliko lengo lingine.
... akiwa na mtoto wake.
Wasafiri wanaingia au kutoka Hispania
wakiwa na zaidi ya Euro 10,000 au kiasi kinachofanana na hicho wanatakiwa kutangaza
chini ya sheria mpya ya kutakatisha fedha chafu na ukwepaji wa kodi iliyoanzishwa mwaka 2007. Tamko hilo linatakiwa kufanywa kwa kujaza fomu kutoka katika mtandao au kutoka hazina na ofisi za ushuru.
Mpaka leo haijulikani kama alirudishiwa fedha hizo au la.
Post a Comment