LONDON,
ENGLAND
MESUT
OZIL yule kiungo fundi wa mpira wa kikosi cha Arsenal, anafikiria mpango wa
kuachana na timu hiyo kama Arsene Wenger ataendelea kuwa kocha msimu ujao.
Kwa
mujibu wa gazeti moja la Hispania, Don Balon, supastaa huyo ghali kwenye kikosi
hicho cha Emirates atafungasha virago vyake na kuondoka kama Mfaransa Wenger
ataendelea kubaki kuwa kocha kwenye kikosi hicho.
Ozil
Imeelezwa
kwamba Ozil amechoshwa na kitendo cha Arsenal kushindwa kuwa washindani kwenye
kusaka ubingwa wa Ligi Kuu na mataji mengine na anadhani jambo hilo kwa kiasi
kikubwa linakwamishwa na kocha Wenger.
Mpango
wa mchezaji huyo ni kurudi Hispania kujiunga na klabu yake ya zamani ya Real
Madrid licha ya kwamba timu nyingine kama Atletico Madrid, Valencia na Sevilla nazo
zimeonyesha nia ya kuhitaji huduma yake.
Ozil na Sanchez
Ikiwa
imebakiza mechi nane kumaliza msimu wa Ligi Kuu England, Arsenal kwa sasa ipo
nyuma kwa pointi 11 dhidi ya vinara Leicester City, hivyo inahitaji kushinda
kila mechi ili kumaliza ukame wa taji hilo uliodumu kwa klabu hiyo kwa miaka 12
sasa.
Kocha
Wenger amelalamikia mashabiki kushindwa kutoa sapoti kwa timu hiyo hasa kwa
kipindi hiki muhimu zaidi katika kumalizia msimu.
Ozil akiwa Madrid
Mchezaji
mwingine wa Arsenal, Alexis Sanchez naye ameshaanza kukumbwa na hali kama hiyo,
huku kukiwa na madai kwamba ana mpango wa kwenda kucheza soka Italia.
Arsenal
imetolewa katika mashindano yote matatu iliyokuwa ikishiri na iko katika nafasi
ngumu kuweza kutwaa Kombe la Ligi Kuu England.
Post a Comment