0


BARCELONA,HISPANIA
LUIS SUAREZ ameng’ara na kuwa katika kiwango kizuri Barcelona msimu huu, tayari amefunga mabao 43, lakini straika huyo anakiri hakuwa na uhakika kama angeweza kukifanya hicho anachokifanya wakati anajiunga na klabu hiyo mwaka 2014.
Staa huyo wa Uruguay amejiunga na miamba hiyo ya Catalunya  akitokea Liverpool kwa ada ya Pauni 75 milioni  na amechukua muda mfupi kuthibitisha thamani yake Nou Camp.
Suarez, Neymar na Messi
Amekuwa akicheza katika jukumu la kufanikisha kutwaa mataji matatu msimu huu, Suarez sasa yuko kwenye kiwango kingine akiwa kama mmoja kati ya wachezaji watatu wanaotisha katika safu ya ushambuliaji duniani.
Suarez, Neymar na bila ya shaka, Lionel Messi, wanaongoza kwa upande wao kurudia mafanikio ya ajabu ya msimu uliopita katika Ligi ya Mabingwa, La Liga na Copa del Rey.
Suarez mwenye umri wa miaka  29 anaweza kujiamini sasa lakini hakuwa hivyo wakati alipofanya uamuzi wa kujiunga na klabu hiyo ya Hispania.
Alisema: “Nilikuwa na ndoto za kuichezea Barcelona, lakini sikuamini kama nilikuwa mzuri wa kutosha kiasi cha kuwa  namba tisa wao.

Suarez
“Kila siku nilikuwa naweza kucheza na timu bora na sasa nacheza na Messi (Lionel), Neymar, (Andres) Iniesta, (Sergio) Busquets na wengine.” 
Suarez alizungumzia uhusiano wake na Messi na Neymar ambao wanatengeneza utatu unaotisha uliopachikwa jina la 'MSN'  alisema: “Hatujari nani anafunga, kitu pekee ni kuona timu inafanya vizuri,” aliongeza. 

...alipojiunga
“Wote tuko sawa kuhusu malengo yetu, ambayo ni kushinda pamoja. Wote tuna furaha- hakuna wivu kati yangu, Neymar na Messi. Kila kitu kinakuja kwa uhalisia wake kati yetu.”

Post a Comment

 
Top