0


MADRID, HISPANIA
CRISTIANO RONALDO inaonekana kama anaumizwa kichwa na mwanaye, Cristiano Jr ambaye anataka awe mchezaji wa soka kama alivyo yeye.

Mshindi huyo wa Ball’on d’Our mara tatu anataka mtoto wake afuate nyayo zake  za kusakata soka lakini anasema hatamlazimisha kufanya hivyo.

...dogo akijifua
Supastaa huyo wa Real Madrid amembaini  mtoto wake  huyo atakuwa mwanamichezo akiwa na umri wa miaka mitano tu.
Ronaldo, 31, alisema: “Nataka mwanangu awe mchezaji. Mimi ni mchezaji wa soka na nataka mwanangu awe hivyo pia.
“Nadhani kuna kitu cha kimichezo kinamhusu, ana sifa za kuwa mwanariadha.
“Bila shaka bado mdogo sana, mtoto, ana miaka mitano anapenda soka, hilo ni jambo kubwa.”
Ronaldo anautumia muda wake  wa ziada nje ya Real Madrid kufanya mazoezi na kijana wake huyo wa kiume  ana anapenda kumuona akija kuwa mchezaji mkubwa kama alivyo yeye.

... akiwa na mwanawe
Lakini Ronaldo hataki Cristiano Jr afikirie sana kwa kuwa baba yake anataka acheze soka na anamtaka kufanya chaguo lake  yeye mwenyewe.
Ronaldo aliongeza: “Nina mipira 30 nyumbani, kila siku anakuwa na mpira na anaupenda. Lakini sitamlazimisha kuwa mchezaji kwa sababu hilo linakuja kwa asili, anatakiwa kufanya chaguo lake.

Ronaldo kazini
“Anaweza kuwa anavyotaka kuwa, sitamlazimisha kabisa.
“Lakini bila shakan nataka  Cristiano awe mchezaji mmoja mkubwa, kama baba yake.”

Post a Comment

 
Top