0


PARIS, UFARANSA
ZLATAN IBRAHIMOVIC straika wa Paris Saint-Germain amethibitisha  amepokea ofa za kwenda kucheza Ligi Kuu ya England mwishoni mwa msimu huu.
Ibrahimovic anatarajiwa kuondoka kuwatumikia mabingwa hao wa Ufaransa  mwishoni mwa msimu wakati mkataba wake utakapofikia mwisho na vita ya kuipata saini yake vitakuwa vya kutisha.

Zlatan
Arsenal na  Chelsea, kama ilivyo kwa West Ham, zimeonesha matamanio ya kutaka kumbakisha staa huyo London, lakini  mchezaji huyo wa kimataifa wa Sweden  amesema atachukua muda wa kufanya uchaguzi.
Akizungumza katika mkutano wa kuelekea mchezo wa kirafiki wa kimataifa kati ya Sweden  dhidi ya Jamhuri ya Czech, Ibrahimovic alisema : “Ndio kuna matamanio ya Ligi Kuu Engkland,  naweza kuthibitisha hilo.

...akiwa mazoezini 
“Ligi Kuu England ni ligi ambayo mashabiki wanaizungumza duniani kote. Vitu vingi vitakuwa sawa pindi nitakapofanya uamuzi mwishoni mwa msimu.
“Pindi muda huo utakapofika, wakati karata zote zitakapokuwa juu ya meza, hapo ndipo nitakapoenda ninapotaka na tutaona nani anayetaka zaidi.
“Ni kama harusi. Pande mbili zinataka, siyo sehemu moja tu au upande mwingine. Kila upande unahitaji zaidi ya mwingine.” 
Pamoja na kwamba uamuzi utakuwa wa Ibrahimovic, West Ham wanaokana wamejipanga  kutoa kiasi kikubwa katika klabu za London pindi litakapoanza suala la mapatano.
Wakati Ibrahimovic anahitaji mshahara wa Pauni150,000 kwa wiki, ukweli ni kwamba anapatikana bure jambo ambalo linaonekana kuwa ni hatari.

... mazoezini na timu ya taifa.
Arsenal itakuwa katika msukumo mkubwa kuhakikisha inamsajili nyota mwenye jina kubwa katika usajili wa majira ya joto- na Ibrahimovic, ambaye anakuwa na thamani ya jumla ya Pauni 133.2 milioni anaonekana kufaa katika mpango huo.
Hata hivyo, Ibrahimovic  pia anaweza kuwindwa na Manchester United kama kocha wa zamani wa Chelsea, Jose Mourinho atachukua mikoba na kumrithi Louis van Gaal mwishoni mwa msimu. 

Post a Comment

 
Top