MANCHESTER,
ENGLAND
SIR ALEX FERGUSON (pichani Juu) ameibuka na kumtetea kocha aliyeko kwenye
wakati mgumu klabuni Manchester United, Louis van Gaal na kuwataka mashabiki
kuwa na uvumilivu pindi klabu inapopita katika wakati mgumu.
Van Gaal
Pamoja na kuwa nyuma kwa pointi moja nje ya nne bora na
kushika nafasi ya sita katika Ligi Kuu England na mchezo mmoja wa marudiano wa nusu
fainali wa Kombe la FA uwanjani Wembley FA, United imetolewa katika Ligi ya
Mabingwa katika hatua ya makundi.
Imetolewa katika Europa League na wapinzani wao wakubwa Liverpool
na imepoteza dhidi ya Middlesbrough katika Kombe la Capital One.
Depay
Kumekuwapo na ongezeko kubwa la machafuko kwa mashabiki kushindwa
kuishangilia timu hiyo na kuizomea kutokana na jinsi Van Gaal anakoipeleka timu
hiyo, lakini Ferguson, ambaye amekuwa
akihudhuria kila mechi za nyumbani na ugenini, amesisitiza mashabiki wasiwe na
tabia ya kuhukumu haraka.
“Wafu ni rahisi kuwa watu muhimu,” alisema.
“Wafu ni rahisi kuwa watu muhimu,” alisema.
“Tunahitaji kuwa wakweli kwa baadhi ya mambo - idadi ya
majeruhi ilikuwa ni, Phil Jones amecheza mechi saba tu msimu huu, Ashley Young,
(Antonio) Valencia, (Luke) Shaw, hii ni hasara kubwa.
“Haijalishi una timu gani, kama unawakosa wachezaji wenye
kariba kama yao unakuwa na hasara kubwa sana kwenye timu.
Martial
“Katika nyanja nyingine ambayo siyo rahisi kusahau pia kuna wachezaji
wapya watano katika kikosi cha kwanza cha United msimu huu, na wawili ni
makinda (Anthony) Martial na Memphis (Depay) na uwezo wao ulikuwa mzuri tu.
“Unatakiwa kuwa na uvumilivu fulani unapokuwa shabiki wa Manchester
United na baadhi yao wameonesha hivyo kwa miaka kadhaa.
Rashford
Moja kati ya mambo mazurui nje ya matatizo ya majeraha ya
wachezaji kwa Van Gaal ni kuibuka kwa baadhi ya wachezaji vijana walioingia
katika timu.
Moja ya ingizo bora lilikuwa ni Marcus Rashford, mzaliwa wa
Manchester mwenye umri wa miakia 18, aliyefunga mabao matano katika mechi nane.
“Mnatakiwa kumpa sifa yake, amewapa nafasi wachezaji tisa
makinda. Nadhani mbele atakuwa vizuri,” Ferguson alisema akimfagilia Van Gaal.
Post a Comment