Lionel Messi
CAIRO, MISRI
LIONEL MESSI
amezua utata Misri baada ya mwanasiasa
mmoja na afisa wa michezo kupandwa na hasira kutokana na mchango wake wa jozi
ya viatu alivyovitoa kwa ajili ya kuchangisha fedha.
Runinga ya
MBC Masr ilitangaza mahojiano na Messi katika kipindi cha 'Yes I am Famous' Jumamosi iliyopita, ambapo nahodha huyo wa Argentina alipotangaza
kutoa jozi ya viatu kwa ajili ya kupigwa mnada.
Kwa
utamaduni wa Misri, kama nchi nyingine za Kiarabu, kuchukua viatu vya mtu
kunatazamwa kama ni matusi. Mbunge wa Bunge la Misri, Said Hassain, ambaye
anamiliki kipindi cha utangazaji alisema: “Viatu vya nani mnavyotaka kuviuza,
Messi? Mnadhani mtapata kiasi gani?
“Hamfahamu
kwamba kucha ya mtoto wa Kimisri ina thamani zaidi ya viatu vyenu? Kaeni na
viatu vyenu au kaviuzeni Israel.”
Hassain aliongeza:
“Messi, sisi Wamisri tuko watu milioni 90, tunajivunia, tuna viatu.”
“Hatuli
kutokana na pesa za viatu vya watu wengine. Ningemwelewa kama angechangia jezi
yake ya Barcelona kwa Wamisri, hiyo inakubalika. Lakini viatu? Hii ni fedhea
kwa Wamisri wote na mimi sikubaliani na fedheha hii. Wamisri hawawezi kutafuta
chakula, lakini wanafahari.'
“Sisi
Wamisri hatujawahi kuwa wanyonge katika miaka yetu elfu saba ya ustaarabu.”
Hassain aliendelea
kwa kumpa nafasi Azmy Megahed ambaye ni msemaji wa Chama cha Soka cha Misri, aliyekuwa
na maoni yake.
“Nimechanganyikiwa. Kama yeye (Messi) alikuwa
na lengo la kutudhalilisha, nasema ni bora akaweka viatu hivi juu ya kichwa chake
na vichwa vya watu wanaomshabikia.
“Hatuna haja
na viatu vyake na hatuna haja na upendo wa watu wa Israeli au Waisraeli. Toa
viatu vyako kwa nchi yako, Argentina imejaa masikini kibao.”
...akiitumikia Argentina
Mona
El-Sharkawy, ambaye ndiye aliyeendesha mahojiano na Messi katika Runinga ya MBC Masr, alimtetea mshindi
huyo mara tano wa tuzo ya Ballon d'Or na
alisisitiza kwamba kitendo hicho kimepokelewa vibaya.
El-Sharkawy
alisema: “Hii ni mbaya sana. Inajenga mwonekano kwamba sisi tunachukua mawazo
ya wageni wetu na kuyaweka katika mnada kwa upendo.
“Nimeshangazwa,
sijasema kama tutatoa viatu hivyo kwa ajili ya michango ya Misri au sehemu
nyingine. Sijui kwa nini wanasema amevitoa kwa ajili ya Misri. Hili halijasemwa
kamwe.”
akishangilia bao la 50.
Messi alifunga bao lake la
50 kwa Argentina katika ushindi wa mabao 2-0 wa kufuzu kwa ajili ya Kombe la
Dunia dhidi ya Bolivia Jumanne usiku, hajatoa
maoni yoyote kuhusu viatu vyake kusababisha hasira hizo.
Post a Comment