Sehemu ya nyumba ya Ronaldo
MADRID, HISPANIA
CRISTIANO RONALDO amesababisha uvumi
wa kuondoka kwake Real Madrid kukuwa zaidi baada ya kuliweka jumba lake la kifahari
sokoni. Imeripotiwa kwamba supastaa huyo wa Ureno yuko mbioni kuhama Bernabeu mwishoni mwa msimu huu.
Mtandano wa Kihispania wa OK Diario umedai kwamba Ronado, 31, anataka kulipiga bei jumba lake hilo la kifahari kwa Pauni 4 milioni lililopo Madrid ikiwa njia mojawapo ya kujiandaa kuondoka.
...akiangalia mabwawa
Pia, anadaiwa kuuza nyumba ya mama yake kwa thamani ya Pauni 2 milioni, ukiwa ni mpango wa familia nzima kuondoka.
Mapema mwaka huu, Ronaldo aliposti video akifanya ziara katika jumba lake la kifahari – akiwapa matumaini mashabiki kwamba hivyo ndivyo vitu ambavyo pesa zinaweza kununua.
Jumba hilo lina vyumba saba vya kulala, mabafu ya kuoga tisa, vyoo vinane, lifti, mabwawa ya kuogelea ya ndani na nje, chumba cha sinema, sehemu ya kufanyia mazoezi ‘gym’, sehemu nane za kuegesha magari na nyumbna ya pembeni ya wafanyakazi.
sebule.
Ronaldo anahusishwa na mpango wa kutaka kurudi katika klabu yake ya zamani ya Manchester United- ambapo Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo, Ed Woodward aliwahi kuweka wazi kwamba klabu yake ina mkakati wa kumsajili mchezaji mwenye kiwango kikubwa cha dunia.
Ronaldo
Na mshindi huyo wa mara tatu wa tuzo ya Ballon d’or anafaa kuwamo katika mpango huyo.
Ronaldo aliondoka Old Trafford na kutua Bernabeu kwa Pauni 80 milioni mwaka 2009 – na United inaweza kuvunja benki kuweza kumrudisha.
...nyumbani kwake.
Hata hivyo, Man United itakuwa katika ushindani mkali na miamba ya Ufaransa wa Paris Saint-Germain ambayo nayo inaweza jina la mchezaji mkubwa kuziba nafasi ya Zlatan Ibrahimovic anayetaka kutua England mwishoni mwa msimu huu.
Post a Comment