Ronaldo na Kate
MANCHESTER, ENGLAND
CRISTIANO RONALDO
aliweka upinzani wa klabu za Real Madrid na Barcelona pembeni na kumsadia, Neymar
katika tuzo za Ballon d’Or Januari, kwa mujibu wa Mtangazaji wa Televisheni,
Kate Abdo.
Kate (kualia) katika majukumu
Nyota huyo wa Real
Madrid alipuuza dharau na matusi ya Nou
Camp wakati timu hizo zinapopambana katika vita ta kuwania taji la Ligi ya La
Liga kwa miaka kadhaa.
Lakini Ronaldo alikuwa
na furaha kutoa msaada wake kwa Mbrazili, Neymar ambaye anakipiga katika klabu
ya Barcelona katika shindano hilo la tuzo za Ballon d'Or lililofanyika Januari.
Ronaldo alishindwa na
Lionel Messi kutwaa tuzo hiyo ya kifahari, wakati Neymar alishika nafasi ya
tatu katika ushiriki wake wa mara ya kwanza.
Neymar katikati akiwa jukwani, kulia ni Kate.
“Katika Ballon d'Or niliyoshiriki Januari, tulifanya mazoezi
kidogo na wachezaji kabla ya kupanda jukwaani,” Ballon d'Or alifafanua Kate
Abdo alipofanya mahojiano.
“Yeye (Ronaldo)
alikuja na Neymar, ambaye ni Mbrazili na Ronaldo ni Mreno, kwa kuwa wote
wanazungumza Kireno, pamoja na Messi na Neymar wanacheza timu moja, alikuwa ni Ronaldo
aliyemchukua na kumuonesha anapotakiwa kwenda, kuhakikisha anamtafsiria kila
kitu.
Ronaldo
“Alikuwa mkarimu na
kuonesha kujali mbele ya Neymar, kwa jinsi alivyokuwa akimwangalia na
kuhakikisha anajua kile anachokifanya. Na huu ni upande mwingine (wa Ronaldo) labda
huwezi kutarajia,” alisema Abdo ambaye ni Muingereza anayetangaza katika
Runinga ya Sky Sports.
Messi alishinda tuzo ya Ballon d'Or kwa
mchezaji bora wa dunia kwa mara ya tano.
Messi alitwaa tuzo
Muargentina huyo
mwenye umri wa miaka 28 alipata 41.33% ya
kura zote, Ronaldo alipata 27.76% na kushika nafasi ya pili na Neymar alipata 7.86% akishkika nafasi ya
tatu.
Post a Comment