ABUJA, NIGERIA
ALEX IWOBI wa Arsenal amelazimika
kutolewa katika mazoezi akiwa na timu yake ya taifa ya Nigeria baada ya kuumwa
kutokana na kula chakula kichafu (foodpoisoning), Kocha wa Nigeria, Samson
Siasia amethibitisha.Iwobi, 19, alikimbizwa hospitali baadaa ya kula saladi akiwa na wachezaji wengine katika mazoezi ya msingi jijini Abuja.
"Aliumwa baada ya kula chakula kichafu na kwa hiyo hakuwamo katika sehemu ya mazoezi," Siasia aliwaambia waandishi wa habari katika mkutano. "Lakini anaendelea vizuri."
Iwobi amecheza michezo miwili ya kirafiki akiwa na Nigeria, aliibukia katika soka la vijana la England kwa kuzichezea timu za Arsenal na timu za taifa za vijana za England kuanzia miaka 16, 17 na 18.
Kinda huyo alitarajiwa kucheza mchezo wake wa kwanza wa ushindani kwa kuitumikia nchi yake ya kuzaliwa katika mchezo wa kufuzu Kombe la Afrika dhidi ya Misri, Ijumaa.
Iwobi aliifungia bao Arsenal katika mchezo dhidi ya Everton uwanjani Goodison Park, Jumamosi iliyopita. Katika mchezo huo Arsenal ilishinda mabao 2-0.
Post a Comment