0
Gary Neville
VALENCIA, HISPANIA
GARY NELVILLE ametimuliwa baada ya miezi minne ya kuitumikia timu hiyo, huku kocha wa zamani, Pako Ayestaran akichukua nafasi yake hadi mwishoni mwa msimu.
Neville, 41, alichaguliwa kukiongoza kikosi hicho katika Ligi ya La Liga Desemba 2 mwaka jana lakini ameshindwa kutimiza malengo ya klabu hiyo. 

...akitoka uwanjani akiwa hoi
Katika michezo 16 aliyoiongoza Valencia, Neville ameshinda mitatu, ametoa sare mitano na kufungwa minane. Klabu hiyo maarufu kama ‘Los Che’ kwa sasa iko katika nafasi ya 14 katikan msimamo, ikiwa na tofauti ya pointi sita juu ya eneo hatari la kushuka daraja.
Mashabiki wa Valencia waliizomea timu hiyo kufuatia kipigo cha mabao 2-0 katika uwanja wa nyumbani dhidi ya Celta Vigo kabla ya mapumziko ya kupisha mechi za kimataifa, na walisikika wakiimba :"Gary ondoka sasa ," wakati mchezo huo ulipokuwa ukiendelea.

Benchi lilikuwa gumu 
Waraka uliotolewa katika mtando wa klabu hiyo ulisomeka hivi: "Klabu ya Valencia leo imeagana na Gary Neville akiwa kama kocha mkuu.

...alitoa mbinu zake zote.
"Baada kuzingatia kwa umakini, klabu imeamua kufanya mabadiliko na kwa maslahi bora ya Valencia CF kusonga mbele msimu huu. Tunamshukuru Gary kwa kufanya kazi Valencia na tunamtakia kila la heri mbele ya safari.
"Klabu leo hii imemchagua Pako Ayestaran kuwa kocha mkuu hadi mwishoni mwa msimu huu.
"Ayestaran alikuwa kocha msaidizi wa Valencia  mwaka 2001 hadi 2004  na aliisaidia kutwaa mataji mawili ya La Liga na Kombe la Uefa.

...alijaribu kujitetea.
“Kuanzia  2004 hadi 2007, alikuwa kocha msaidizi wa Liverpool FC, klabu hiyo ya Uingereza ilishinda  taji la Ligi ya Mabingwa 2004-05 na Kombe la FA mwaka 2006.
"Akiwa kama kocha mkuu, Ayestarán alishinda  na klabu ya Maccabi Tel-Aviv (kombe la ligi na makombe mengine mawili) na pia alifundisha México akiwa na Santos Laguna na  Estudiantes Tecos (mabingwa wa  mashindano ya Clausura)."


 

Post a Comment

 
Top