0


MONTEVIDEO, URUGUAY
LUIS SUAREZ ataitumikia timu yake ya taifa ya Uruguay katika mchezo dhidi ya Brazili baada ya kumaliza adhabu ya kukosa michezo tisa kutokana na kumng’ata beki, Giorgio Chiellini.
Straika huyo wa Barcelona alimng’ata Chiellini  katika mchezo wa Kombe la Dunia, uliofanyika Brazil na alisisitiza hana tena mpango wa kuonesha tabia mbaya katika michezo atakayocheza.

...akimng'ata Chiellini
Straika huyo ataichezea timu yake ya taifa kwa mara ya kwanza tangu alipofanya kosa hilo mwaka 2014 katika mchezo dhidi ya Italia.
Suarez alimng’ata Chiellini begani katika mchezo mgumu uliochezwa Natal na akahukumiwa kukosa michezo tisa ya kimataifa.

                                     Suarez mazoezini na Uruguay
Anarudi uwanjani dhidi ya Brazil katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia za 2018, Ijumaa hii.
"Natarajia kuwa na tabia ileile, bado nitakimbia, nitatoa upinzani, bado nitakuwa mbishi kwa sababu hakuna mtu anayeweza kunibadilisha jinsi ninavyocheza," alisema.
"Lakini kwa kasi, kama ninavyofanya sasa Barcelona, nitakuwa mjanja kwa vitu vingi, nikijaribu kufanya mambo yenye faida na kuyapa kipaumbele

...akiwa Uruguay
" Kitu pekee ninachotaka ni kuichezea tena timu yangu ya taifa kwa mara nyingine na kufurahia joto la mashabiki."
Uruguay ilianza vizuri katika kuwania kufuzu kwa fainali hizo baada ya kushinda michezo mitatu kati ya minne na kushika nafasi ya pili katika timu10, nyuma ya Ecuador, ambayo imeshinda michezo yao yote mpaka sasa.

... akiwa na Barcelona.
Baada ya mchezo dhidi ya Brazil ambayo inaongozwa na staa mwingine wa Barcelona, Neymar, Uruguay itarudi nyumbani kupambana na Peru, Jumanne ijayo.
Suarez amekuwa katika wakati mzuri akiwa na Barcelona msimu huu baada ya kufunga mabao 26  katika michezo 28 ya Ligi ya La Liga ya Hispania.

Post a Comment

 
Top