0




ABUJA, NIGERIA

ALEX IWOBI staa wa Arsenal mwenye umri wa miaka 19 ambaye aliitumikia England katika kadhaa za timu za vijana kabla ya kuchagua kuitumikia timu kubwa ya Nigeria, ametoka hospitali.

Iwobi ameruhusiwa kutoka hospitali na yuko tayari kwa ajili kuitumikia Nigeria katika mchezo dhidi ya Misri.
Timu ya Taifa ya Nigeria, maarufu  ‘Super Eagles’ itaikaribisha  Misri  Ijumaa hii  katika mchezo wa kuwania kufuzu kwa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika na kulikuwa na wasiwasi kwamba Iwobi – aliyelazwa kutokana na kula chakula kichafu ‘food poisoning’ – asingeweza kucheza mchezon huo.

Lakini  kinda huyo wa  Arsenal amewataka watu kufuta mawazo hayo kwa kuandika katika Mtandao wake wa  Twitter: "Nilikula chakula kichafu ‘food poisoning’ lakini niko vizuri sasa na ninafikiria niko tayari kwa ajili ya mchezo dhidi ya Wamisri."
Kocha wa Nigeria, Samson Siasia alithibitisha kutokea kwa tukio hilo  la mchezaji huyo kukimbizwa hospitali akitokea mazoezini baada ya kula saladi.
Iwobi alikuwa na uwezo wa kuchagua kuzitumikia timu mbili za taifa kati ya England na Nigeria lakini aliamua kuitumikia timu ya Afrika ambako ndiko alikozaliwa baada ya kuvikataa vishawishi vya England.

Post a Comment

 
Top