MANACHESTER, ENGLAND
JOSE MOURINHO atapewa ofa nene ya
Pauni 60 milioni ili aweze kuirudisha Manchester United katika makali yake. Kiasi hicho ni kikubwa zaidi, kuliko Pauni 15 milioni kwa mwaka ambacho Manchester City imepanga kumpa Pep Guardiola atakapoanza kazi mwishini mwa msimu huu.
Kiasi hicho kitajumuisha pamoja na bonasi ya kushinda mataji ya Ligi Kuu na makombe mengine, kitamfanya Mourinho kuwa kocha anayelipwa zaidi katika historia.
Mourinho
Kiasi hicho kitakuwa ni mara mbili
ya kile anachokipata Louis van Gaal kwa sasa. Kuna makubaliano maalumu
yatakayomfanya Mourinho kuanza kuitumikia klabu hiyo Mei. Bosi huyo Mreno na washauri wake wameshawishika na dili hilo, ambalo litamfanya kuingiza Pauni 20 milioni kwa mwaka.
Imekuwa hamu ya muda mrefu ya Mourinho kufundisha Old Trafford. Kocha huyo alishangazwa wakati alipopuuzwa kupewa nafasi hiyo, pale Alex Ferguson alipostaafu na neema ikamwangukia David Moyes.
Kocha huyo maarufu kama ‘Special One’ alitwaa taji la Ligi Kuu akiwa na Chelsea msimu uliopita lakini alifukuzwa Desemba 17 mwaka jana.
Kumekuwa
na maelezo kwamba Mourinho atakuwa mrithi wa Mdachi huyo kwenye kikosi hicho
cha Old Trafford baada ya kushindwa kuifanya timu hiyo kuwa na makali
yaliyotarajiwa licha ya kupewa pesa za kutosha kufanya usajili.
Mourinho
anaamini kazi ya kuinoa Man United msimu ujao ni yake hata kama Van Gaal
ataiwezesha timu hiyo kumaliza ligi ndani ya nafasi nne za juu na kufuzu
kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.
Guardiola
Kwa
pesa ambazo Van Gaal alitumia kwenye kusajili nyota wapya, Man United ilipaswa
kwa sasa kugombea ubingwa na si kuhangaikia nafasi ya nne ili kuwamo kwenye
Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.
Mourinho
anaamini kwa pesa za klabu ya Man United zinampa fursa ya kutosha kutafuta
wachezaji anaowataka na kurudisha heshima ya klabu hiyo yenye maskani yake Old
Trafford.
Post a Comment