MANCHESTER,
ENGLAND
MEMPHIS DEPAY hana budi kujipanga na
kukubaliana na kweli kwamba hatakuwa mchezaji wa Manchester United baada ya mwishoni
mwa msimu huu. Man United itasikiliza ofa kwa staa huyo iliyemnunua kwa mbwembwe kwa Pauni 25 mwaka mmoja uliopita kutoka katika klabu ya PSV ya Uholanzi.
Mbali na Depay nyota mwingine atakayeondoka ni Morgan Schneiderlin akiwa na msimu mmoja tu tangu awasili akitokea Southampton.
Inadaiwa kuwa Schneiderlin ameshindwa kuonesha kiwango alichokuwa nacho Southampton tangu ametua Old Trafford.
Na mabeki Phil Jones na Marcos Rojo wapo shakani kuendelea kuitumikia United ambayo iko katika harakati za kutengeneza kikosi chake upya.
Bosi Louis van Gaal kibarua chake kiko shakani huku Jose Mourinho akiwa anasubiria kuchukua nafasi yake.
Depay, 22, alitarajiwa kuleta changamoto katika safu ya
ushambuliaji ya United lakini kiwango chake kimeshuka sana na kuwakatisha tamaa United.
Staa huyo wa kimataifa wa Uholanzi alipewa jezi namba saba ambayo
huwa inavaliwa na mastaa wanaoaminiwa katika klabu hiyo.
Schneiderlin
Wengi walitarajia Depay angekuwa Cristiano Ronaldo mwingine
lakini matumaini yamekuwa tofauti.
Mashabiki wa United uwanjani Old Traffod msimu huu walikuwa
wakipiga kelele za “shambulia, shambulia, shambulia” baada ya timu hiyo chini
ya Van Gaal kuonekana kushindwa kufanya hivyo, huku Depay akionekana kushindwa kitendo kilichoonekana kama aibu kwake.
Jones amekuwa akisumbuliwa na majeraha msimu huu na ameanza
katika michezo sita ya mwisho ya Ligi Kuu tangu Januari.
Romero
Rojo pia amekuwa akisumbuliwa na
majeraha ya bega na amerudi katika michezo saba ya mwisho baada ya kuwa nje kwa
miezi mitatu. Kipa namba mbili, Sergio Romero yuko njiani kujiunga na River Plate baada ya kushindwa kupata namba mbele ya David de Gea.
Makamu wa Rais wa River Plate Matias Patanian alisema: “River Plate kila siku imekuwa ikivutiwa na wachezaji wazuri - na Romero ni mmoja kati yao.”
Post a Comment