LIVERPOOL,
ENGLAND
CHRISTIAN
BENTEKE ameweka wazi maisha yake ya mateso ndani ya Anfield na kukiri kama
angejua asingejiunga na klabu hiyo. Straika huyo Mbelgiji mwenye umri wa miaka, 25, ametoa dokezo zito kwamba atajaribu kuondoka mwishoni mwa msimu baada ya kupoteza mwelekeo.
Ni Andy Carroll tu aliyenunuliwa kwa Pauni 35 milion na kuigharimu Liverpool Pauni 32.5 milioni ambazo kocha wa zamani wa klabu hiyo, Brendan Rodgers alilipa kumchukua Benteke kutoka Aston Villa mwaka jana.
Lakini ameutumia muda wake mwingi kukaa benchi tangu kocha Jurgen Klopp alipoanza kuifundisha timu hiyo Oktoba mwaka jana.
Sasa
Benteke anasisitiza kwamba angeliyajua hayo mapema asingeipa nafasi ya kwanza
Liverpool kwa kusaini nayo mkataba.
Alisema: “Nisingeweza kusaini kama ningejua siyo chaguo la kwanza
la kocha.” “Kila kitu kilikuwa wazi kwa mimi kucheza na kuwa na msimu mzuri katika klabu kubwa kama nilivyoanza vizuri.
“Nilikuwa wa kwanza kukubali kuonesha thamani yangu ya kutosha kwa timu kama Liverpool.
“Katika hatua nyingine, chini ya Rodgers, nilijua ningepata nafasi ya kuonesha kiwango changu.
“Nilikujua ningepata nafasi ya kuonesha thamani ya fedha nilizosajiliwa na ninastahili kuvaa jezi ya Liverpool.
“Lakini tangu nimekuja England mwaka 2012 sijakaa benchi kwa kipindi kirefu kama hiki. Inaumiza, ikizingatiwa kwamba sijawahi kuwa fiti kama nilivyo hivi sasa.
“Hiyo ndiyo sababu huwa ninataka kupora nafasi yangu pindi ninapopata dakika tano au kumi za kucheza. Sitaki watu wanilaumu.”
Benteke anasema ni vigumu kuelewa kwa nini Klopp anampuuza na kumweka benchi.
Alisema: “baadhi ya wachezaji wenzangu walisema nina bahati kwa ujio wa Klopp, kwa sababu nitacheza mara kwa mara.
“Pindi kocha anaposema alitaka kukuchukua alipokuwa Dortmund na baada ya muda mnakuwa katika timu moja na anakupuuza ni vigumu kuelewa.
“Nimecheza mechi mbili tu mfululizo tangu Klopp amewasili. Nilichezaa dhidi ya Leicester, nikafunga bao, ikafuatia dhidi Sunderland nikafunga na tukapoteza kwa West Ham na baada ya hapo nikaondolewa.”
Benteke alianza katika mechi mbili tu tangu January 2 mwaka huu za Kombe la FA dhidi ya Exeter na West Ham.
Wakosoaji wa mshambuliaji huyo wa zamani wa Aston Villa wanasema anapata shida Liverpool kwa sababu kocha Klopp anapenda mchezo wa pasi.
Benteke alisema: “Sioni ajabu, sielewi kwanini watu wanasema hivyo.
“Ninaweza kucheza kwa kupasia na kukimbia. Hatuchezi staili kama ya Barcelona.”
Kutokana na hali hiyo, mchezaji huyo alipata ushauri kutoka kwa wachezaji wenzake wa timu ya taifa ya Ubelgiji, Eden Hazard na Marouane Fellaini ili kujaribu kufufua morari wake.
Marafiki zake hao, waliwahi kukutwa na hali kama hiyo wakiwa Chelsea na Manchester United msimu huu, na wamejaribu kumfariji.
Aliongeza: “Hata baba yangu ambaye ameanza kuwa na hofu na heshima yangu, aliniambia kuwa sitaweza kufanya chochote kutokana na hali ilivyo.
“Nilizungumza na Eden na Marouane, nao wamenishauri hivyohivyo – kama kocha hakupangi huwezi kufanya vya kutosha kuhusu hilo.”
Uhusiano wake na mashabiki wa Liverpool umeshuka sana.
Benteke alisema : “ Pamoja na hali hiyo, bado ninashika nafasi ya pili kwa ufungaji kwenye timu, baada ya Roberto Firmino, mwenye maboa manane.
“Hii siyo mbaya, ingawaje nilitarajia zaidi. Kukosolewa pia kunatokana na kwamba mimi ni mgeni.
"Januari sikutaka kuondoka, tamaa yangu ni kupata mafanikio nikiwa na Liverpool. Nataka kuendelea kuwepo.Lakini mwishoni mwa msimu tutafanya mahesabu.”
Post a Comment