0


NEW YORK, MAREKANI
CRISTIANO RONALDO yuko katika vita ya kisheria akidaiwa kununua nyumba  juu ya  Trump Towers kwa ajili ya rafiki yake mchezaji wa kickboxer, Mmorocco, Badri Hari.
Ronaldo wiki iliyopita alidai kampuni ya samani ya Kiitaliano ililihusisha jina lake kwa makosa katika mikataba ya New York na hoteli jijini Monaco.

Hari akiwa amembeba Ronaldo
Lakini  Kampuni ya Proto Enterprises imepanga kufungua kesi na kudai Pauni 7.8 milioni dhidi ya staa huyo wa Real Madrid, ikisitiza staa huyo alinunua maghorofa yaliyopo Fifth Avenue kama zawadi kwa rafiki yake wa karibu, Badr Hari.
Kampuni hiyo imesema Jumatatu imewasilisha malalamiko katika Mahakama ya Madrid kwa madai ya kashfa na kutoa taarifa ya uongo.

sebule
Hari na Ronaldo wamekuwa na urafiki wa karibu kwa zaidi ya mwaka sasa, huku staa huyo wa Real Madrid akiripotiwa kufanya ziara za mara kwa mara kumfuata rafiki yake huyo Afrika.

Mojawapo ya chumba
Wawakilishi wa Ronaldo wiki iliyopita walianza mchakato wa kufungua kesi dhidi ya Kampuni ya Proto Enterprises, ambayo inaongozwa na tajiri, Alessandro Proto.

Sehemu ya korido
Malalamiko ya wawakilisha hao ni kuhusiana na kampuni hiyo kumhusisha kimakosa na mlolongo wa mipango staa huyo likiwemo ghorofa lenye thamani ya Pauni 11.8 milioni katika jengo linalomilikiwa na mgombea urais wa Marekani Donald Trump.

Trump Tower
Waraka uliotolewa wiki ilioyopita ulisema: “Jina na heshima ya Cristiano vimekuwa vikitumika mara kadhaa na kampuni hiyo kutoa taarifa za uongo, zimewafanya kufungua kesi  katika mahakama ya Italia.”
Lakini Kampuni ya Proto imejitokeza na kusema kwamba sababu kubwa iliyomchukiza staa huyo ni kuweka hadharani ghorofa alilipanga kulitoa kwa rafiki yake.

Ronaldo
Kampuni hiyo ilisema: “Madai na kashfa ya kutoa taarifa za uongo dhidi ya Ronaldo yamefanyika. Tumeomba kulipwa Euro 10 milioni kwa kudaiwa kusema uongo.
“Baada ya kuandikisha faida ya majengo, tulitakiwa na mamlaka kuweka wazi kwamba tumeuza ghorofa kwa Ronaldo aliyelitoa kwa rafiki yake Mmoroco, Hari.
“Labda hicho ndicho kinachomsumbua mchezaji huyo ambaye kabla ya hapo hakusema kitu chochote kuhusu mananunuzi hayo. Tunasubri majibu yake.

Ronaldo na Karim Benzema.
“Samahani kwa kuweka hadharani siri ya Ronaldo, lakini sheria za Marekani ni kali sana, na sisi tumetimiza wajibu wetu. Malalamiko dhidi ya Ronaldo, kwa maneno haya dhidi ya jamii yetu, yameshafanyika na kuwasilishwa.”

Mgombea uraisi wa Marekani, Trump.
“Rais Mtarajiwa wa Marekani, Trump ni mshirika wa kibiashara wa Kampuni ya Proto,” uliendelea kuweka wazi waraka huyo ukiwa na sahihi yake: “Ronaldo anakabiliwa na ugumu fulani katika maisha binafsi, na hili kwa kiasi fulani lina athari kwa miasha yake. Lakini tunapaswa kulinda heshima yetu.”
Vyumba vitatu (apartment), vilijengwa mwaka 1983, vinaonekana kama moja ya sehemu za kifahari zaidi katika Jiji la Manhattan na sehemu ya kujivunia kwa watu maarufu duniani.

Post a Comment

 
Top