BRASILIA,
BRAZILI
RONALDINHO
bado hajakata tamaa pamoja na kushindwa
kwenda na kasi yake ya zamani, nyota huyo amepanga kwenda kumalizia maisha yake
ya soka kucheza soka katika Ligi Kuu ya Marekani au China.Supastaa huyo mwenye umri wa miaka 36 aliachwa na klabu ya Brazili ya Fluminense, Septemba mwaka jana na amekuwa akisaka klabu nyingine ya kuchezea tangu kipindi hicho.
Na wakala wake, Roberto Assis, ambaye pia ni kaka yake, amethibitisha kwamba Mbrazili huyo atakwwenda kucheza Marekani au China.
Ronaldinho
Assis alisema: " Sehemu mwafaka kwake
kutua ni katika Ligi ya Marekani ‘Major League’ (MLS) au Ligi Kuu ya China."
Pamoja na
kutokuwa na timu kwa nusu mwaka, nyota
huyo wa zamani wa Barcelona bado anataka kulipwa mshahara mnono.
Januari, Newcastle United ilishindwa
kumchukua Ronaldinho kutokana na bei kubwa baada ya wakala wake kusisitiza kuwa
ana thamani ya Pauni 6 milioni kwa
mwaka. Lakini MLS na Ligi Kuu ya China zote huwa zinatoa mishahara minono kwa nyota ambao wana umri mkubwa.
Nyota kama Kaka, Andrea Pirlo, David Villa na Steven Gerrard
wote wanacheza Marekani baada ya kutengeneza pesa nyingi wakitokea Ulaya.
Ronaldinho
Kama ilivyo kwa Ligi Kuu ya China ambayo hivi karibuni
imewachukua Jackson Martinez, Ezequiel Lavezzi na Ramires.
Ronaldinho alishinda tuzo ya Ballon
d'Or, Ligi ya Mabingwa na Kombe la Dunia
enzi zake akicheza soka la ushindani katika soka la Ulaya, ambapo alizitumikia PSG,
Barcelona na AC Milan. Kitendo cha kuweka wazi matamanio yake, kutamfanya mchawi huyo wa Samba kuwindwa timu za Ligi za MLS na ile ya China ambazo zinataka kutengeneza zaidi wasifu wao.
Post a Comment