0


MANCHESTER, ENGLAND 
MANCHESTER CITY inajipanga kukifanyia mabadiliko makubwa  kikosi chake mwishoni mwa msimu chini ya bosi mpya Pep Guardiola lakini nahodha, Vincent Kompany hatauzwa.
Man City inaamini ujio wa Guardiola unaweza kuwarudisha katika Ligi ya Mabingwa kwa mara nyingine, na hata kuweza kutwaa ubingwa huo, baada ya kupotea njia katika mbio za ubingwa msimu huu.
Tangu Guardiola alipotangazwa kujiunga na Man City, mkurugenzi wa michezo wa klabu hiyo, Txiki Begiristain amekuwa akipokea simu kutoka kwa mawakala wa wachezaji kutoka England, Hipsania, Italia na Ujerumani, wakiwa na wasiwasi na wateja wao kama watapata nafasi ya kucheza chini ya kocha huyo mpya.

Begiristain atafanya kazi sambamba na Guardiola.
 Pamoja na Man City kufanya vibaya, na kwa mujibu wa rekodi za mafanikio za Guardiola, Man City ina matumaini anaweza kurudisha makali yao. Ikiwa chini ya kocha Manuel Pellegrini, Man City iko nyuma kwa pointi 15 kwa vinara wa Ligi Kuu, Leicester.
Viongozi wa Man City pia wanaamini Guardiola anaweza kujenga umoja uwanjani Etihad, sambamba na mafanikio yake aliyoyapata Barcelona na Bayern Munich.
Pamoja na kwamba Guardiola ameingia mkataba wa miaka mitatu na klabu hiyo, matajiri wa Kiarabu wanaoimiliki timu hiyo wanaamini anaweza kuongeza mkataba Etihad mara mbili zaidi kama atarudia mafanikio aliyoyapata Barca.

Mangala ameshindwa  kazi
Wakati Guardiola akitarajiwa kukifumua kikosi cha Man City mwishoni mwa msimu, na wachezaji wanne au watano wakitarajiwa kutemwa na wengine kuchukua nafasi zao, nahodha Kompany hayumo katika listi ya wachezaji watakaoachwa.
Kompany yuko nje ya kikosi kwa mara ya nne msimu huu kutokana na kuumia kifundo cha mguu, huku akihofiwa kuwa na umri wa miaka 29, beki huyo hawezi kuondolewa kutokana na tatizo analopambana nalo msimu huu.
Matajiri wa Man City wamemhakikishia Kompany kwamba watakuwa naye na kutatua tatizo lake na kumwezesha kung’ara chini ya Guardiola.

siku zake zinahesabika, Etihad
Hata hivyo, beki aliyesajiliwa kwa Pauni 42 milioni, Eliaquim Mangala ataachwa mwishoni mwa msimu, sambamba na beki, Martin Demichelis, kutokana na kuonesha uwezo mdogo msimu huu.
Pamoja na kwamba, maisha ya baadaye ya Yaya Toure hayajulikani, imefahamika kwamba hakuna mambo binafsi kati yake na Guardiola, pamoja na kwamba bosi huyo wa zamani wa Barca alimuuza kiungo huyo kwenda Man City.

Yaya hana bifu binafsi na Guardiola.
Man City imekanusha madai kutoka kwa wakala wa Toure, ya kutakiwa kumpa mchezaji huyo mkataba wa miaka mitatu, na imaanini kiungo huyo mwenye umri wa miaka 32 anaweza kuwa muhimu chini ya utawala wa Guardiola msimu ujao.

Bado anahitajika.
Raheem Sterling, ambaye amekuwa akipambana kuonesha uwezo wake msimu wake wa kwanza Man City kufuatia kununuliwa kwa Pauni 49 milioni kutoka Liverpool katika msimu wa majira ya joto uliopita, pia atapewa muda kuthibitisha thamani yake chini ya Guardiola.

Raheem, anatakiwa kuonesha thamani yake.
Pamoja na kuanguka katika vita ya kuwania taji la Ligi Kuu msimu huu, na kubakia kupambana  kushiriki Ligi ya Mabingwa, Bodi ya Man City ina matumaini Guardiola atairudisha timu hiyo katika makali yake. Kocha huyo atapewa mamlaka makubwa zaidi kuliko yake aliyonayo Bayern Munich, ambapo kiungo Toni Kroos aliuzwa kwenda Real Madrid bila ya maagizo yake mwaka 2014.
Akiwa Man City, Guardiola atafanya kazi karibu na Begiristain, ambaye amekuwa akiufurahia uhusino wake tangu alipokuwa naye Barca, kwa kutoa  uamuzi mchezaji gani anatakiwa kusajiliwa na yupi anafaa kuuzwa.

Toni Kroos, aliuzwa bila ya ridhaa ya Guardiola.
Man City ina matumaini makubwa na Shule yao ya Michezo (Academy) yenye thamani ya Pauni 200 milioni, ambayo ina vipaji vya kutosha na  inaamini wachezaji wa kikosi cha kwanza katika miaka mitano ijayo watatokea hapo, wakiwa kama wale wa Barcelona waliotokea katika Academy ya La Masia, kina Lionel Messi, Andres Iniesta na Xavi.

Post a Comment

 
Top