LEIRIA, URENO
CRISTIANO RONALDO amekosa penalti wakati Ureno ikipoteza
mchezo wa kimataifa wa kirafiki kwa bao 1-0 dhidi ya Bulgaria katika uwanja wa
nyumbani mjini Leiria Jumamosi.
Ronaldo alikosa nafasi ya kusawazisha bao hilo katika
kipindi cha pili ikiwa ni penalti yake
ya tatu kukosa katoka umbali wa yadi 12 kwa klabu na nchi yake – huku bao la Bulgaria
likipachikwa na Marcelinho.
Bulgaria imeshindwa kufuzu kwa Euro 2016, inapaswa
kumshukurukipa wake, Vladislav Stoyanov kutokana na ushindi huo.
Stoyanov akidaka penalti ya Ronaldo.
Stoyanov aliokoa mabao ya wazi kutokana na mashambulizi ya
Ureno – mara mbili kutoka kwa Ronaldo na Nani.
Marcelinho aliipatia Bulgaria bao
hilo pekee katika dakika ya 19. Ronaldo
staa wa zamani wa Manchester United sasa amekosa penalti tatu kati ya nne
alizopiga hivi karibuni.
Ronaldo
ambaye amekuwa akikimbilia kupiga penalti kila zinapopatikana ama kwenye timu
yake ya taifa au klabu, katika kipindi cha miezi mitatu ya hivi karibu amepiga
penalti nne na kufunga moja tu.
Ronaldo akimtoka beki.
Mmoja
kati ya makipa waliodaka penalti za Mreno hiyo ni Mcamerooni, Idriss Carlos
Kameni kwenye mechi kati ya Malaga na Real Madrid iliyofanyika Februari 21
uwanjani La Rosaleda.
Marcelinho akishangilia bao lake
Penalti
pekee aliyofunga Ronaldo ni ile kwenye mechi dhidi ya Levante iliyofanyika
mwanzoni mwa mwezi huu.
Mikwaju
mingine ya penalti aliyokosa ni dhidi ya Sevilla uwanjani Bernabeu na hii ya juzi
dhidi ya Bulgaria kwenye mechi ya kirafiki ya kimataifa ambapo kipa Stoyanov
alipangua mkwaju huo.
Post a Comment