0
Terry akinyanyua Kombe la Ligi Kuu
LONDON, ENGLAND
BEKI na nahodha wa Chelsea, John Terry ataondoka katika timu hiyo mwishoni mwa msimu huu baada ya kutangaza usiku wa Jumapili iliyopita kwamba Chelsea imekataa kumuongezea mkataba mpya.
Beki huyo mwenye umri wa miaka 35 aliweka wazi hatima yake hiyo baada ya ushindi wa mabao 5-1 wa Kombe la FA raundi ya nne dhidi ya MK Dons.
Terry

Terry alisema atamaliza enzi zake baada ya kuitumikia Stamford Bridge kwa maika 21, hata hivyo aliweka wazi kwamba hatajiunga na klabu nyiingine ya Ligi Kuu England.
Nahodha huyo alisema alipendelea kuitumikia Chelsea lakini aliambiwa na maofisa wa klabu katika mkutano kabla ya mchezo dhidi ya Arsenal wiki iliyopita kwamba hawatamuongezea mkataba.
Hata hivyo, Chelsea imesisitiza kwamba mjadala kuhusu kuondoka au kubaki kwa beki huyo uko wazi
Beki huyo amekuwa kama nembo ya kwenye klabu  hiyo tangu alipokuwa na umri wa miaka 14 na alifurahia maisha yake kwa kushinda mataji manne ya Ligi Kuu, makombe matano ya FA, makombe matatu ya ligi, Kombe la Ligi ya Mabingwa na Kombe la Ulaya. 

Akishangilia bao alililofunga
Terry anataka kuendelea kucheza lakini ameahidi hatajiunga na timu nyingine yoyote ya Ligi Kuu England, huku akisubiri ofa ya kutoka China ai Marekani.
“Hautakuwa mwisho wangu wa kucheza, sitaachana na soka Chelsea,” Terry alithibitisha. 
“ Huu ni msimu wangu wa mwisho wa Kombe la FA kwa hiyo nataka kuufanya kuwa wa kukumbukwa. Ni msimu mzuri kwangu na nataka kuendalea kufanya vizuri – sio kwenye mashindano hayo tu hata kwenye Ligi Kuu.”
Pamoja na kupata mafanikio akiwa Stamford Bridge, Terry pia amekutana na matatizo mbalimbali. Mwaka  2010, alifikishwa Mahakama Kuu na kusababisha kuondolewa unahodha wa timu ya taifa ya England, kwa kosa la kuwa na uhusiano  wa kimapenzi na mpenzi wa mchezaji wa zamani wa Chelsea, Wayne Bridge.

Terry
Miaka miwili baadaye, alifungiwa michezo minne na kupigwa faini ya Pauni 220,000 na FA baada ya kukutwa na hatia ya kumfanyia vitendo vya ubaguzi beki wa QPR, Anton Ferdinand.
Kesi hiyo ilisababisha Terry kumaliza harakati zake za kucheza michezo ya kimataifa pamoja na kuondoka kwa kocha wa timu ya taifa ya England, Fabio Capello.

Post a Comment

 
Top