0
Van Gaal
MANCHESTER, ENGLAND
LOUIS VAN GAAL anatakiwa kuirudisha Manchester United  katika Ligi ya Mabingwa Ulaya kama anataka kuendelea na kibarua chake Old Trafford.
Tofauti na ilivyokuwa kwa Sir Alex Ferguson mwaka 1990, aliposhinda Kombe la FA. Msimu huu hilo haliwezi kumnusuru Mdachi huyo kufukuzwa Old Trafford.
Hisa za United katika soko la hisa la New York, zimeshuka kwa kisi kikubwa, Pauni 320 milioni zimekuwa zikipotea katika soko hilo katika miezi sita iliyopita.

Kiasi cha kuwafanya wamiliki na wawekezaji kutaka kufuzu katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Hiyo inamaanisha, Van Gaal anapaswa kumaliza katika nne bora ‘Top Four’katika Ligi Kuu England au kushinda Ligi ya Europa, ambayo kwa sasa huzipa hadhi klabu za Ulaya kushiriki mshandano makubwa.
Kocha huyo alipata faraja, Ijumaa iliyopita baada ya kuifunga Derby County katika Kombe la FA katika mchezo wa raundi ya nne.
Van Gaal amekuwa akisakamwa na mashabiki wanaotaka afukuzwe kwenye kibarua chake.
Mashabiki kama hao ndio waliokuwa wakimtaka kocha Alex Ferguson afukuzwe miaka 26 iliyopita.
Lakini ushindi wa Mark Robins kwa Nottingham Forest ulimpa Ferguson muda – na United ilienda kubeba kombe baada ya kucheza mchezo wa marudiasno dhidi ya Crystal Palace.
Hocho kilikuwa kichocheo kwa Fergie kupitia katika mafanikio makubwa katika historia ya klabu hiyo.
Lakini kwa Van Gaal, matarajio ni tofauti.
United haijashinda taji la FA kwa miaka 12 na kwa kubeba kombe hilo la fedha kutamfanya Mdachi huyo afungashiwe virago. Kwa sababu haitaweza kuwatuliza Wamarekani hao wa United.
Wakazi hao wa Mji wa Florida-familia ya Glazers watakabiliwa na madeni ya Pauni 411milioni.
Hiyo ndio sababu kocha David Moyes kufukuzwa baada ya miezi minane Machi 2014 baada ya kupatikana uhakika kuwa United isingeweza kumaliza katika nne bora msimu huo.
Kukosa kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya kuliifanya kupoteza kiasi cha Pauni 38 milioni.
Na baada ya kumpa, Van Gaal Pauni 250 milioni kufanya usajili wa wachezaji wapya, familia ya Glazers itakuwa vigumu kuendelea na ukarimu wa kukosa mapato ya Ulaya kwa mwaka wa pili katika misimu mitatu.
Kama United itakosa kushiriki tena mwaka huu, itapoteza kiasi kikubwa cha fedha hususan kwenye dili la televisioni msimu ujao.
Hiyo itaifanya United kuwa klabu ya kwanza kupoteza mapato ya Pauni 500 milioni kwa mwaka na kuondoka katika hadhi ya kuwa klabu kubwa katika kuingiza mapato katika michezo yake. Lakini pia hisa zao zitaanguka.
Pindi United ilipoibuka na ushindi wa bao1-0 dhidi ya Tottenham mwezi Agosti, hisa katika soko la biashara la New York zilikuwa 18.37.

Katika kufunga biashara Ijumaa jioni, kufuatia ushindi huo wa Pride Park, hisa zilishuka hadi Dola 15.67.
Hiyo inaanisha thamani ya hisa katika klabu imeshuka kutoka Pauni 2.15 bilioni hadi Pauni 1.83 bilioni. Van Gaal ameshinda ligi katika nchi za Uholanzi, Hipsania na Ujerumani. Lakini matumaini yake ya kutwaa taji la Ligi Kuu England yamefifia haraka, na anaweza kuokoka kama atafuzu nne bora au kushinda Ueropa Ligi.
Tofauti na hapo Van Gaal apoteza nafasi ya kuutetea mkataba wake  na nafasi yake atapewa msaidizi wake Ryan Giggs.

Post a Comment

 
Top