0
Guardiola
MANCHESTER, ENGLAND
SAHAU kabisa kuhusu siku ya mwisho ya usajili. Huu ni usajili wa msimu.
Pep Guardiola amesaini mkataba wa miaka mitatu kuitumikia Manchester City baada ya kocha Manuel Pellegrini kuthibitisha kuwa ataondoka mwishoni mwa msimu  huu.
Pellegrini alivunja ukimya katika mkutano na waandishi wa habari Jumanne usiku akiwa Sunderland, wakati Man City ilipokuwa ikijadiliana na Guardiola kuhusu kuifundisha timu hiyo tangu mwaka 2012.

Tamaa ya Man City kumtaka Guardiola imewekwa hadharani  kupitia walaka maalumu uliotolewa Jumatatu ukithibitisha kwamba kocha huyo atajiunganga na klabu hiyo.
Pellegrini alisema Man City haikumzunguka na walaka huyo ulisomeka hivi: “Manchester City inathibitisha kwamba katika wiki za hivi karibuni itaanza majadiliano ya mkataba na Pep Guardiola ili kuwa kocha mkuu  wa Manchester City kwa ajili ya msimu wa Ligi Kuu England wa 2016/17 na kuendelea.
“Mkataba huo utakuwa wa miaka mitatu. Majadiliano haya yaliaanza na kukatizwa mwaka 2012.

Pellegrini
“ Kwa heshima ya Manuel Pellegrini na wachezaji, klabu imeweka hadharani uamuzi huo kuondoa tetesi zisizokuwa na ulazima.
“Manuel, ameunga mkono uamuzi huo kwa kufanya mawasiliano na bado yuko makini katika kutimiza malengo yake kwa msimu unaoendelea na amekuwa na heshima na dhamira ya dhati kwa wote waliohusika  na kwa uongozi wa klabu.”
Pellegrini anaondoka akiwa na uhakika kwamba Manchester City ikiwa katika nafasi nzuri katika mashindano mbalimbali ya msimu huu.
Klabu hiyo iko katika nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu England, ikiwa pointi tatu nyuma ya Leicester City, imeshinda michezo 13 kati ya 23 ya ligi msimu huu.
Aidha Man City imeingia fainali ya Kombe la Capital One ambapo itacheza na Liverpool, ikitaka kushinda kombe hilo mara ya pili katika miaka mitatu. 
 Guardiola kocha wa zamani wa Barcelona ambaye kwa sasa anakionoa kikosi cha Bayern Munich ya Ujerumani hivi karibuni alikaririwa akisema kuwa atakwenda kufanya kazi katika Ligi Kuu England.



Post a Comment

 
Top