0
Patrick Vieira
Vieira akiwa na Arsenal 
Wenger

NEW YORK, MAREKANI
ULITEGEMEA kulisikia hili? Kiungo mkongwe wa zamani wa Arsenal, Patrick Vieira amedai kwamba kocha, Jose Mourinho ni bora kuliko Arsene Wenger.
Viera raia wa Ufaransa, 39, wiki hii alitangazwa kuwa kocha mkuu wa  klabu ya New York City FC katika Ligi ya Marekani ya MLS.
Pamoja na kuchukua mataji tisa chini ya kocha Wenger akiwa na Arsenal, Vieira bado amempa hadhi kubwa kocha aliyefukuzwa kazi Chelsea, Jose Mourinho.
Alipoulizwa ni nani atakayekuwa kocha wa kikosi chake cha kufikirika ‘Dream Team IX’, alisema: “Jose. Ni kocha mwenye ushawishi kwangu.
“Arsene (Wenger) amejilimbikiza kwenye timu yake. Yeye anatoa uhuru wa wachezaji kujieleza. Ni mtindo tofauti.”
Vieira alishinda mataji matatu ya Ligi Kuu na Makombe manne ya FA katika kipindi chake akiwa Kaskazini mwa London, ukiwemo na ushindi wa Arsenal katika msimu wa 2003/04 wa Ligi Kuu ambapo timu hiyo ilichukua ubingwa bila ya kufungwa.
Viera ambaye alishinda Kombe la Dunia akiwa na timu yake ya taifa ya Ufaransa mwaka 1998, baadaye alikwenda Italia kujiunga na Juventus na baadaye Inter Milan, ambapo alikutana na Mourinho.
Na pamoja na kwamba aliachwa na Mreno huyo baada ya miezi 18 18 pale San Siro, Vieira alidai alijifunza mengi katika kipindi hicho tofauti na alipokuwa chini ya Wenger.
Akizungumza na  Gazeti la Times, Viera aliongeza: “ Ni mmoja kati ya makocha ambao walinishawishi zaidi kutokana na maadili yake ya kazi.
“Anajua kila kitu kuhusu timu pinzani, nguvu yao na udhaifu wao.
“Uwezo wake ulikuwa wa kustajabisha – Kila alichokitaka kutoka kwa kila mchezaji kilikuwa wazi.
“Sijui ni nini kimetokea Chelsea lakini kila siku alikuwa akipata kilicho bora kutoka kwa wachezaji wake.”
Vieira alimalizia kusakata soka katika klabu ya Manchester City, kabla ya kupewa jukumu la kukiendeleza kikosi hicho.
Kwanza alipewa kazi ya ukocha kwa kukifundisha kikosi cha Man City chini ya miaka 21na sasa anakinoa kikosi cha Marekani NYCFC.

Mourinho
Vieira kwa muda mrefu amekuwa akichukuliwa kama atakuwa mrithi wa Wenger, Emirates, lakini amebainisha kwamba bosi wake huyo wa zamani hakuwahi kumwambia chochote.
Alisema: “Sijawahi kuwasiliana na mtu yeyote kwa ajili ya kuongoza au kuhusishwa kwenye klabu.
“Nilikuwa nategemea kitui fulani kutoka kwao, lakini hakikutokea. Hakijaniumiza.”
“Yeye (Wenger) ni mtu ambaye kila wakati yuko bize. Sijazungunmza naye kwa muda mrefu sana.


Post a Comment

 
Top