Pep Guardiola
MANCHESTER, ENGLAND
MANCHESTER United imefanya umafia wa kumnasa
kocha Pep Guardiola kutoka kwa mahasimu wao Manchester City baada ya kukutana
naye kwa siri nchini Ufaransa.
Maofisa wa Man United wamekutana ana kwa ana na
Guardiola kwa ajili ya mazungumzo mjini Paris, Ufaransa wiki iliyopita, kwa
mujibu wa Gazeti la L’Equipe.
Kikao hicho cha siri kilifanyika kwenye hoteli
ya nyota tano ya Le Bristol.
Usiku wa juzi Alhamisi, maofisa wa Man United
walikana kukutana na kocha huyo, lakini ripoti hiyo imeishtua Man City, ambao inadhani Mhispaniola huyo atakuwa kocha wao kuanzia msimu ujao.
Guardiola, 45, ameshatangaza hadharani kwamba
kibarua chake kijacho kitakuwa England kwa maana kwamba ataachana na
Bayern Munich mwishoni mwa msimu huu.
Lakini, kocha huyo hakuwa tayari kusema kwamba
atatua Man City japo ya kuwapo na ripoti kwamba amekubaliana kwa mdomo tu.
Man United inaamini staili ya Guardiola
itawafaa kabisa kwenye kikosi chao na kwamba atarejesha heshima ya Old
Trafford.
Post a Comment