Kocha anayedaiwa kuwaniwa na Chelsea, Max Allegri
Kocha wa muda wa Chelsea, Guus Hiddink.
CHELSEA inadaiwa kumpa nafasi ya kwanza kocha, Max Allegri ya kukinoa kikosi chao mwishoni mwa msimu huu.
Klabu hiyo ambayo kwa sasa inanolewa na kocha wa muda Guus Hiddink imefanya mawasiliano na wawakilishi wa kocha Allegri anayeinoa Juventus mwanzoni mwa mwezi na bilionea Roman Abramovich ameonyesha umakini katika hatua hiyo ya kutafuta kocha mpya.
Wakati wa majadiliano, Allegri alikubali kuchukua
makujumu hazo mazito Stamford Bridge na kufanya kazi katika timu hiyo ya Ligi
Kuu England.
Muitaliano
huyo mwenye umri wa miaka 48, ameshinda mataji mawili ya Serie A moja akiwa na AC
Milan na lingine na Juventus na ameipeleka Juve katika fainali ya Ligi ya
Mabingwa Ulaya na kufungwa na Barcelona. Kwa kufanya mazungumzo na Allegri, Chelsea imepunguza kasi ya kumuwinda kocha wa Atletico Madrid, Diego Simeone baada ya kufanya utafiti na kuwa na mashaka kama Muargentina huyo atakubali kuondoka katika timu hiyo.
Pia bilionea, Abramovich amekuwa na wasiwasi na staili ya Simeone ya kupenda kujilinda na kudai kuwa inafanana sana na ile ya kocha Mourinho aliyemtimua kazi.
Kwa upande mwingine, Allegri ana heshima na mkarimu na kuamini kuw anaweza kufanya kazi na klabu hiyo. Chelsea pia imemuondoa katika mawazo yake kocha anayeondoka Bayern Munich, Pep Guardiola kwa kuamini kuwa ana nia ya kutua Man City.
Post a Comment