0

MANCHESTER, ENGLAND
KOCHA wa Manchester United, Louis Van Gaal amesema kamwe hawezi kuandika barua ya kujiuzulu katika nafasi yake katika klabu hiyo.
 Alizungumza maneno hayo mbele ya waandishi wa habari kabla ya mchezo wa Ijumaa wa raundi ya tano ya Kombe la FA dhidi ya Derby County.
Bosi huyo wa Manchester United amekanusha taarifa mbaya kuhusu mustakabali wake kwamba aliandika barua ya kujuzulu kuifundisha timu hiyo.
Presha ya Van Gaal kufukuzwa iliongezeka Old Trafford kufuatia kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Southampton Jumamosi iliyopita.

Wachezaji wa Man United wakiwa wamekata tamaa baada ya kufungwa na Southampton
 “Sidhani kama nilifanya hivyo kamwe. Mmetengeneza habari yenu. Kisha natakiwa kuijibu. Sijafanya hivyo,” alisema.
 Kocha huyo alisema yeye ni mpiganaji na hataomba kuachia ngazi katika nafasi ya ukocha Manchester United.
“ Kila siku ninapambana. Ni wajibu wenu, mimi kama kocha na wachezaji tutasimama tena kutokanana kile mlichokifanya kwa kuwa ni taaluma yenu.
“Kila siku huwa inakuwa kama hivi ninapopoteza mechi labda katika dakika za mwisho, mnachosha. Jinsi tulivyocheza dhidi ya Southampton siyo kila siku ni habari kubwa, kwa sababu unaweza kucheza vibaya na ukashinda.
“Pindi hali hiyo inapotokea huwa mnachosha. Lakini tumecheza vizuri sana na tumepoteza, kama mchezo wa Chelsea ugenini msimu uliopita, kwa hiyo hali hiyo inapojitokeza mnachosha zaidi kuliko kitu kingine.”
“Ni mara ya tatu sasa (mnaandika) nimefukuzwa na bado niko hapa.

Van Gaal alidaiwa kuandika barua ya kuchia ngazi kwa Makamu Mwenyekiti wa Manchester United, Ed Woodward.
Van Gaal alisema: 'Sitafanya hivyo, milele. Mchango wa Woodward ni mkubwa na hauna shaka, lakini pia unawapa nyie presha kubwa.
“Pindi Bodi inapokuwa na uhakika presha inakuwa kubwa sana kuliko pale inaposema tunakupa mchezo wa mwisho.
“Kujiamini kwako kunapokuwa siyo kwa uhakika, unaweza kupambana na hali hiyo,” alisema  kocha huyo.




Post a Comment

 
Top