0
Firmino
 Firmino.
LIVERPOOL, ENGLAND

IMEELEZWA kwamba mchezaji wa Liverpool, Roberto Firmino aliyenunuliwa kwa Pauni 29 milioni msimu majira ya joto yuko kwenye kiwango sawa na kina Mesut Ozil, Andres Iniesta na David Silva.
Kauli hiyo imetolewa na Ronaldinho ambaye amemtaka kocha Jurgen Klopp kuijenga Liverpool kupitia kwa Roberto Firmino.
Nyota huyo wa zamani wa Barcelona, amesema Mbrazili mwenzake Firmino ni mmoja kati ya namba 10 bora dunia.
Klopp anapanga kukitengeneza upya kikosi alichokirithi kutoka kwa Brendan Rogers Oktoba mwaka jana katika usajili wa majira ya joto, na Ronaldinho amemwambia bosi huyo wa Liverpool kuwasajili wachezaji watakaosaidana na Firmino.
"Sitaki hata kujiuliza kama atakuja kuwa mchezaji mkubwa wa Liverpool, ninajua atakuwa tu," alisema mchezaji huyo aliyewahi kushinda Kombe la Dunia.
"Ni mmjoja wa wachezaji bora kutokana na kile anachokifanya duniani. Yuko katika kiwango sawa na Ozil, Silva, Iniesta, na wachezaji wote wakubwa wanaocheza kwenye katika kiwango kama hicho.
"Ni mchezaji ambaye ninaamini Klopp ataijenga Liverpool mpya kupitia kwake.


Ronaldinho
"Klopp ni kocha bora duniani, anafahamu Liverpool inahitaji wachezaji bora, atajua kwamba Firmino anahitaji wachezaji bora wamzunguke kufanya vizuri kwenye mchezo.
"Nina uhakika wakati, Klopp akijiunga na Liverpool aliahidi kuwasajili wachezaji wake, na Firmino akiwa katikati ya timu, hakuna sababu kwa nini Liverpool isitoe ushindi tena."
Firmino mwenye umri wa miaka  24, aliisaidia Liverpool kufikia fainali za Capital Cup katikati ya wiki na sasa itakunana na Manchester City.

 

Post a Comment

 
Top