0
Kombe la Ligi Kuu England.

LONDON, ENGLAND

KAMPUNI ya Kimarekani imeifanya utafiti wa kila mechi iliyobaki katika Ligi Kuu England msimu huu na kutoa matokeo kwamba Arsenal itaibuka bingwa.

Pamoja na kwamba iko nyuma kwa pointi tatu kutoka kwa vinara wanaoongoza ligi hiyo, Leicester, Arsenal ina asilimia tatu zaidi ya Manchester City kuweza kukwea kileleni.
Lakini bahati mbaya kwa mashabiki wa Manchester United, ambao kwa mujibu wa utafiti huo wataikosa kwa mara nyingine Ligi ya Mabingwa Ulaya huku Tottenham na Leicester zikiingia katika Top Four.
Kwa mujibu wa ripoti, Leicester ina wastani wa 4.4 asilimia kumaliza katika nne bora – chini ya 5.6 asilimia za Spurs.
Man United ina wastani wa 48 asilimia kuweza kuingia Top Four, ikiwa imeanguka kwa pointi mbili  nyuma ya Leicester kuweza kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Na pamoja na kuwa na msimu mbaya, Chelsea imepata wastani mbaya wa 3.3 asilimi kuweza kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Chini ya msimo wa Ligi Kuu England, Aston Villa haiwezi kuepuka kushuka daraja. Utafiti unaonyesha klabu hiyo ina wastani wa asilimia 99 kushuka daraja.
Sunderland itaifuata Aston Villa katika katika mkumbo huo wa kushuka daraja. Huku Norwich na Newcastle nazo zikiwa katika hali mbaya kuepuka kushuka daraja.
Katika Ligi Kuu Hispania, Barcelona imepewa asilimia 84.8 kutwaa ubingwa huku Bayern Munich ikipewa asilimia 99.3 kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Ujerumani.
Wababe wa Ufaransa, PSG ambao wanaongoza ligi hiyo kwa tofauti ya pointi 21, wamepewa asilimia 99.9 ya kutwaa ubingwa wakati Juventus ya Italia imepewa asilimia 61.4 kutwaa taji la Ligi Kuu Italia.
Katika Ligi ya Mabingwa Ulaya ambayo inatazamiwa kuendelea kutimua vumbi mwezi ujao, Bayern Munich chini ya kocha mtaalamu, Pep Guardiola, imepewa asilimia 23.5 kutwaa ubingwa huo huku Barcelona ikipewa asilimia 22 kutetea taji lao.
Katika timu za England ni Manchester City ndio ambayo imepewa nafasi ya kufanya vizuri katika michuano hiyo, lakini ikipewa asilimia za chini zaidi. City imepewa asilimia 10.3 tu ya kutwaa ubingwa huo wa Ulaya.

Msimamo wa Utafiti uko hivi:
1.   Arsenal, 74.8 points
2.   Manchester City, 74.1
3.   Tottenham Hotspur, 68.3
4.   Leicester City, 67.1
5.   Manchester United, 65.1
6.   Liverpool, 61.2
7.   Chelsea, 56.5
8.   West Ham United, 54.5
9.   Southampton, 53.2
10.     Stoke City, 51.6
11.  Everton, 51.3
12.Crystal Palace, 50.1
13.  Watford, 47.2
14.West Bromwich Albion, 43.6
15.                     Swansea City, 42.4
16.                     AFC Bournemouth, 38.7
17.                     Newcastle United, 37.7
18.                     Norwich City, 37.6
19.                     Sunderland, 33.4
20.                     Aston Villa, 27.
 

Post a Comment

 
Top