Mourinho na Van Gaal
Van Gaal na Mlourinho
MANCHESTER,
ENGLAND
LOUIS VAN GAAL atawekwa
kiti moto na waandishi wa habari ikiwa ni mara ya kwanza tangu timu yake ilipofungwa
na Southampton, huku ikidaiwa kuwa kocha Jose Mourinho amekubali kuchukua
nafasi kesho.
Kesho
mchana, Van Gaal atajibu maswali kutoka kwa waandishi wa habari na kufafanua
hatma yake ya Manchester United.
Bosi
huyo wa United atakutana na uso kwa uso na waandishi wa habari katika mkutano
huo kabla mchezo wa Kombe la FA dhidi ya Derby utakaopigwa Ijumaa.
Mara
ya mwisho Van Gaal kulazimishwa kujibu maswali magumu ya waandishi wa habari ilikuwa kabla ya Sikukuu ya Krismasi ambapo kulikuwa
na wasiwaji juu ya hatma yake Old Trafford.
Hata
hivyo, katika mkutano huo alijibu maswali matatu tu kabla ya kuondoka mkutanoni
na kumfanya kutumia dakika nne na sekunde 58.
Kocha
huyo bado yuko katika wakati mgumu kufuatia timu yake kufungwa bao 1-0 dhidi ya Southampton.
Kuna
taarifa Mholanzi huyo ana uhakika wa kuendelea kukitumikia kibarua chake hadi
mwishoni mwa msimu huu.
Gazeti
la Italia, Tutto Mercato limeripoti wiki hii kwamba kocha aliyetimuwa Chelsea, Jose
Mourinho amekubali kumrithi Van Gaal Old Trafford.
Hiyo
ilifuatia taarifa zilizotapakaa kutoka ndani ya Man United kwamba, Van Gaal alitaka kuachia ngazi.
Taarifa ambazo zilikanushwa na United.
Man
United inadaiwa imehairisha mpango wake wa kumtimua kocha huyo japokuwa mambo
yake bado magumu Old Trafford.
Inafahamika
kwamba baada ya mapito yote haya, familia ya Glazers inayomiliki klabu hiyo, itakuja
na uamuzi mmoja wa kumchagua Mourinho na kumpa dili la muda mrefu.
Post a Comment