0
Pato
 Pato akiitumia Brazili.
 Pato AC Milan.
LONDON, ENGLAND

ALEXANDRE PATO ametua katika Uwanja wa Ndege wa Heathrow na moja kwa moja kwenda Stamford Bridge kwa ajili ya kukamilisha usajili wake wa kuitumikia Chelsea.
Straika huyo wa Kibrazili mwenye umri wa miaka 26, ametumia saa 11:30 kwa ndege kutoka Sao Paulo.
Pato atafanyiwa vipimo vya afya leo na kama atafuzu ataweza kucheza dhidi ya MK Dons katika  Kombe la FA Jumapili.
Awali, ilidaiwa kuwa Pato alitakiwa kujiunga na timu hiyo kwa mkopo lakini  sasa usajili huo utakuwa wa kudumu na kuhusisha karibu Pauni 7 milioni. Inadaiwa mchezaji  huyo amekubali kusajili dili la miaka mitatu na Chelsea akitokea Corinthians.
Kabla ya usajili huo, Pato alikuwa akitakiwa na timu kadhaa za Ligi Kuu England zikiwemo Liverpool na Tottenham.
Pato alisema: Nina furaha. Nitakuwa hapa sehemu ya ndoto yangu. Chelsea ni nyumba yangu mpya, asante Chelsea kwa kunisapoti, asanteni mashabiki wangu.

Pato uwanja wa ndege
" Ninahitaji kucheza. Siwezi kusema nina furaha kwa kiasi gani leo. Nina shauku. Nataka kuwajua marafiki zangu wapya, wachezaji na timu. Nataka kucheza kwa ajili ya Chelsea."

Pato alitengeneza jina lake akiwa na AC Milan ya Italia, ambako alifunga mabao 63  katika michezo 150 na  kutwaa ubingwa wa Ligi ya Serie  mwaka 2011.  
                                                    Atua London
Baada ya kufunga mabao 26 akiwa kwa mkopo na timu ya  nyumbani kwao Sao Paulo mwaka jana, Pato sasa yuko tayari kucheza katika Ligi Kuu ya England.
                                         Safari ya Stamford Bridge.
Kitendo cha Pato kujiunga na Chelsea kitatoa changamoto kwa straika Diego Costa, aliyefunga bao lake la nane la ushindi katika Ligi Kuu Jumapili iliyopita dhidi ya Arsenal.
Pia, straika huyo ataongeza upinzani kwa Loic Remy na Radamel Falcao ambao wanapigania namba Stamford Bridge. 
 

Post a Comment

 
Top