Remires akiwa Chelsea
LONDON, ENGLAND
NYOTA wa Brazili wa Chelsea, Remires amekamilisha uhamisho wa kushtukiza kwa kuhamia katika Ligi Kuu ya China baada ya kudumu Stamford Bridge kwa miaka mitano.
Chelsea imethibitsiha kuondoka kwa kiungo huyo.Mbrazili huyo amekamilisha uhamisho huo wa kushtukiza na kuhamia katika klabu ya Jiangsu Suning kwa dili la Pauni 25 milioni.
Oktoba mwaka jana, Ramires alisaini mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia Chelsea kwa miaka minne lakini amekubaliwa kuondoka Stamford Bridge.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 28 alijiunga na Chelsea mwaka 2010 na alitoa mchango mkubwa katika Ligi ya Mabingwa mwaka 2012 ambapo timu yake ilitwaa ubingwa huo.
Pia, alichangia timu yake kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya England msimu uliopita na ameanza katika michezo 15 kuwania ubingwa msimu huu.
Dili hilo litamkutanisha Ramires na mchezaji wa zamani wa Chelsea, Dan Petrescu ambaye ni kocha mkuu wa timu hiyo. Pia mchezzaji huyo anafuata nyayo za wachezaji wengine kina Gervinho, Demba Ba na Paulinho ambao wamehamia kwenye soka la Bara la Asia.
Kwa kuondoka kwa Remires, kuinaifanya Chelsea kukamilisha haraka dili la kumchukua kiungo mshambuliaji Alexandre Pato ambaye leo anafanyiwa vipimo vya afya.
Aidha klabu za Newcastle, Crystal Palace, Swansea na Aston Villa zimejiweka tayari kumchukua mshambuliaji mwingine wa Chelsea, Loic Remy kufuatia ujio wa Pato.
Post a Comment