0
Van Gaal akirudi Manchester
Van Gaal alipokuwa akiondoka.

MANCHESTER, ENGLAND
LOUIS VAN GAAL alienda Uholanzi baada ya kipigo cha bao 1-0  katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Southampton, na sasa anaangalia mchezo unaokuja dhidi ya Derby County.
Kocha huyo amerudi Makao Makuu ya Manchester United Carrington kuendelea na kibarua chake katika maandalizi ya mchezo unaofuata ambapo timu hiyo itakuwa ugenini.
Mholanzi huyo alichukua mapumziko ya siku mbili na kuzitumia kwenda Uholanzi kwenye sherehe ya kuzaliwa kwa binti yake. Van Gaal yuko kwenye kiti moto na alirudi England usiku wa Jumatatu.
Habari zinasema Van Gaal ana uhakika wa kibarua chake kufuatia kukingiwa kifua na Makamu Mwenyekiti wa Manchester United, Ed Woodward ambaye anataka kocha huyo aendelee kuifundisha timu hiyo hadi mwishoni mwa msimu.
Lakini zomeazomea inayoendelea Old Trafford inaonyesha kwamba ukarimu wa mashabiki kwa kocha huyo umefikia mwisho.
Wachezaji wa Man United pia walipewa siku mbili za mapumziko baada ya kipigo hicho cha Jumamosi.
Baadhi ya mashabiki wamelalamikia hatua hiyo wakisema timu inatakiwa kuongeza juhudi katika mazoezi kutokana na matokeo na siyo kupunguza.
Hata hivyo, inasemekana mapumziko hayo yalipangwa na klabu hiyo mapema, ili kuwapa muda wachezaji kupumzika baada ya pilikapilika za msimu wa sikukuu.
Man United imekanusha kwamba mapumziko hayo yamekuja baada ya Van Gaal kuomba kujiuzulu kufuatia kipigo ilichokipata timu hiyo kutoka kwa Southampton.
Ripoti zinasema Mholanzi huyo aliomba kuachia ngazi baada  ya kukata tamaa kutokana na kipigo hicho na kitendo cha United kupiga shuti moja tu langoni kwa adui katika dakika 90 minutes.

Post a Comment

 
Top