0


Suarez

BARCELONA, HISPANIA
LUIS SUAREZ ameahidi kama atarudi kucheza soka Ligi Kuu  England atarudi katika klabu yake ya zamani ya Liverpool tu.
Na nyota huyo wa Barcelona amewafagilia mashabiki wa klabu hiyo ya Anfield alipokuwa alipofanya mahojiano na ESPN.
Suarez alishinda tuzo ya mchezaji bora wa kulipwa (PFA) akiwa na Liverpool mwaka 2014, alisema: “Huwezi kujua ni nini kitataokea mbele ya safari, lakini kama nitarudi  England itakuwa ni kwa ajili ya Liverpool na siyo kwa timu nyingine.
“Nimewa-misi sana mashabiki wao. Hali ya hewa ni ya ajabu sana.


 “Kila mmoja aliyeichezea Liverpool anajua umuhimu wa mashabiki. Wanajua wako ndani ya moyo wangu.” Suarez kwa sasa anaongoza katika ufungzaji katika Ligi ya La Liga, ambao Barcelona ilifika kileleni Jumamosi baada ya ushindi dhidi ya Malaga 2-1.

Post a Comment

 
Top