Guardiola
MANCHESTER,
ENGLAND
PEP
GUARDIOLA ametoa majibu ya maswali magumu kuhusu timu gani atatua baada ya kuondoka
Bayern Munich.Ikumbukwe kocha huyo alikaririwa akisema kuwa atakwenda kufundisha England lakini bado hajafanya makubaliano na klabu yoyote.
Guardiola na mkewe
Lakini jana Jumamsi mkewe Cristina Serra amenaswa akipewa hadhi ya VIP katika ziara aliyoifanya katika Shule ya St Bede, Manchester.
Mke huyo wa Guardiola alikuwa ameambatana na mke wa Mkurugenzi wa Man City, Txiki Begiristain katika shule hiyo ambayo ina uhusiano wa karibu na klabu ya Man City.
Karibu asilimia 40 ya wachezaji wa academy ya Man City ni wanafunzi wa St Bede na katika shule hiyo kuna kanisa ambalo kocha wa zamani wa City, Roberto Mancini alitumia kuomba siku moja kabla ya kucheza mchezo wa kihistoria dhidi ya QPR mwaka 2012 QPR, na kuipa ubingwa wa Ligi Kuu.
Guardiola ni baba wa watoto watatu, wa kwanza ni wa kiume Marius, 13, na wanaofuata ni wa kikke Maria (11) na Valentina miaka saba.
Watoto hao hawataweza kushindwa kuvutiwa na kiwango cha elimu na vifaa vya elimu katika shule hiyo.
Uwepo wa mke huyo katika shule hiyo ni hatua mojawapo kuonyesha kwamba Guardiola atakuwa bosi wa Man City kumrithi Manuel Pellegrini.
Imeshathibitishwa kuwa, Guardiola ataondoka Bayern Munich mwishoni mwa msimu, pia alikuwa akitakiwa na wapinzani wa klabu hiyo, Man United, Chelsea na Arsenal.
Guardiola atakuwa kocha wa Man City na kukutana na viongozi wa zamani wa Barcelona Begiristain na Afisa Mtendaji Mkuu, Ferran Soriano.
Pellegrini ameshinda taji la Ligi Kuu na Kombe la Capital One katika miaka yake miwili na nusu katika klabu hiyo.
Guardiola atakaa kwenye kiti moto, Man City kuanzia Juni, huku kukiwa na ripoti kutoka Ujerumani katika Gazeti la Bild kwamba ataingiza mfukoni Pauni 20 milioni kwa msimu.
Post a Comment