0
Falcao amesema bahati mbaya ndiyo inayomtesa siyo majeraha
....amesema goti lake siyo tatizo 
 Kocha wa Chelsea, Guus Hiddink: Majeraha ya Falcao ni makubwa.
LONDON, ENGLAND
RADAMEL FALCAO amesema anapaswa kulaumiwa kwa bahati mbaya aliyonayo Chelsea msimu huu na siyo kutokana na majeraha.
Straika huyo wa Colombia alijiungana Chelsea kwa mkopo akitokea Monaco na amefunga bao moja tu katika michezo 11 akifuatia hali kama hiyo ya kukatisha tamaa iliyomtokea akiwa kwa mkopo Manchester United msimu uliopita ambako alifunga mabao manne.
Pamoja na kusumbuliwa na maumivu ya goti kabla ya kwenda Old Trafford, Falcao alisema hiyo siyo sababu ya kuwa na kiwango kibovu.
Falcao alifanya mahojiano na magazine Semana kwao Colombia alisema:“Nimepona maumivu ya goti langu. Tatizo ni kwamba tangu hapo sijapata nafasi ya kucheza msimu wote ili kurudisha kujiamini na kutoa ushindani tena.
“Kama ningekuwa napata muda huo mara kwa mara wa kucheza soka, msingekuwa mnasema maneno hayo hadi sasa.
“Siwezi kujidhoofisha mwenyewe. Watu wanazungumza sana, lakini baadhi yao wanasema mambo mazuri juu yangu na nimejaribu kupokea ujumbe wote kwa sababu wananipa moyo na ndio kitu ninachokiangalia.”
Hata hivyo, Flacao alisema majeraha yake ya sasa hayahusiani na goti, pamoja na kwamba, kocha wa Chelsea, Guus Hiddink alisema hivi karibuni kuwa majeraha yake ni makubwa sana.
“ Kila mmoja yuko huru kutoa mawazo yake lakini nadhani mwandishi wa habari wanatakiwa kufanya wajibu wao. Wamekosa ukweli,” alisema Falcao.
“Siku hizi hawaendi kwenye chanzo kuthibitisha habari na wanaandika vitu visivyokuwa vya ukweli. Kitu pekee ambacho hawajasema ni kwamba Falcao anakwenda kucheza katika timu nje ya dunia.”



 

Post a Comment

 
Top