0


BARCELONA, HISPANIA
LUIS SUAREZ amelibwatukia Shirikisho la Soka la Dunia la Fifa kwa kutomjumuisha kwenye tatu bora ya sherehe za tuzo ya Ballon d’Or zilizofanyika Uswisi mwezi uliopita.
Staa huyo wa Barcelona hakuhudhuria sherehe hizo zilizofanyika baada ya kutojumukishwa kwenye hatua hiyo ya tatu bora ambayo iliwajumuisha mastraika wenzake wa Barcelona, Lionel Messi, Neymar na straika wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo.
Messi aliibuka kuwa mshindi wa tuzo hiyo na kumfanya kuwa mchezaji aliyeichukua tuzo hiyo mara tano.
Na Suarez anadhani kutochaguliwa kwakwe kwenye tuzo hizo ni kutokana na fikra mbaya juu yake kutoka kwa bodi ya shirikisho hilo.

Suarez alisema: “Fifa walinialika kwenye tuzo za Ballon d’Or huku wakiniomba radhi wakisema kuwa hawakunijumuisha kwa kuwa nilishachaguliwa kuwa mchezaji bora wa Kombe la Dunia la Klabu.
“ Sidhani kama walishawahi kumwalika mshindi wa tuzo hiyo kabla yangu na hiyo imetokea kwa kunialika mimi.”
Straika huyo wa Uruguay amekuwa na historia mbaya na Fifa baada ya shirikisho hilo kumfungia miezi minne na kumpiga faini ya Pauni 65,000 baada ya kumng’ata beki wa Italia, Giorgio Chiellini  katika Kombe la Dunia mwaka 2014.
Akizungumza huku akijitingisha, Suarez alisema: “Ni mashindano ambayo nimeyapenda  na sikufikiria nim nani aliyekuwa akiyandaa.”
Straika huyo wa zamani wa Liverpool alijiunga na Barcelona kwa dau la Pauni 75 milioni wakati akitumikia kifungo hicho amekuwa na wakati mzuri Nou Camp msimu huu, na kudhaniwa kwamba angekuwemo katika hatua tatu bora ya tuzo hizo.
Lakini mabao yake 29 katika michezo 29 yameonekana kama vile hayakutosha kumpa nafasi hiyo.

Post a Comment

 
Top