0


Javier Mascherano akiondoka mahakamani, Barcelona
Mascherano 
Wakili wa Mascherano aliomba mteja wake alipe faini badala ya kutumikia kifungo.
 Mascherano akiwa mahakamani ambako kesi yake ilisikilizwa kwa dakika 10.



BARCELONA, HISPANIA
JAVIER Mascherano wa Barcelona amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela na kupigwa faini ya Pauni 625,000 baada ya kukutwa na makosa mawili ya kukwepa kulipa kodi.
Hata hivyo, hakupendezwa na kutumikia kifungon hicho cha mwaka mmoja, baada ya wakili wake, David Aineto kuomba faini iwe mbadala wa kifungo hicho.
Sheria za Hispania zinaruhusu watu wanaofungwa kifungo cha chini ya miaka miwili wasitumikie kifungo, isipokuwa wale wanaokutwa na hatia ya uhalifu wa kutumia nguvu.
Mascherano, 31, amekutwa na hatia na kuhukumiwa kwenda jela kwa vifungo vya miezi minne na miezi minane kutokana na makosa hayo mawili yalitokea mwaka 2011 na 2012.
Beki huyo wa Muargentina ameshalipa deni la Pauni 1.15 milioni la mamlaka ya kodi kabla ya hajahukumiwa.
Pia, Mascherano ameshalipa riba kwa kiasi hicho cha pesa, lakini anatakiwa kulipa faini mpya.
Makosa aliyokumbana nayo kiungo huyo wa zamani wa Liverpool ni kushindwa kutangaza mapato kutokana na haki ya picha zake kupitia makampuni anayomiliki yaliopo Ureno na Marekani. 
Mascherano alichapisha barua ya wazi baada ya uamuzi huo na kusisitiza kuwa yeye ni mtu mwadilifu na mwenye majukumu.
Aliandika: “Mimi ni mchezaji wa kimataifa, sina ufahamu mkubwa wa masuala ya kodi na yale ya kisheria. Kwa hiyo ninahitaji kusaidiwa na watu wenye ufahamu wa masuala hayo, ambayo kwangu ni magumu.
“ Katika kazi yangu nimekuwa mwadilifu na mtu mwenye majukumu, nikiwaheshimu wachezaji wenzangu, klabu ninayoitumikia na nchi ambayo ninaishi.
“ Hali hii ninayopitia inanipa uzoefu mwingine, kutokana na hili nitatoka nikiwa na nguvu mpya, na nitakuwa mkarimu kama nilivyo kwenye sheria. 

Mascherano akiwa uwanjani.
“Ninahifadhi uwezekano wowote dhidi ya wale walionishauri vibaya kwa kunishauri kitu ambacho hakikuwa sahihi.”
Mascherano siyo nyota pekee wa Barcelona aliyekumbana na matatizo kama hayo, Lionel Messi alishafikishwa mahakamani yeye na baba yake mwezi Mei kutokana na kesi kama hiyo.
Aidha Septemba, nyota mwingine wa Barcelona, Neymar vifaa vyake vyenye thamani ya Pauni 30 milioni vilizuiwa baada ya kushtakiwa kwa kutolipa kodi yake yote.


Post a Comment

 
Top