LONDON, ENGLAND
PACHA ya Arsenal katika Ligi Kuu England
haiko mbali na ile ya Barcelona 'MSN' katika viwango vya safu za mastraika
zilizofanikiwa ligi za Ulaya.
Safu ya Mabingwa wa Ligi ya Ulaya,
Barca inaundwa na Lionel Messi, Luis Suarez na Neymar inaonekana kuwa safu bora
ya ushambuliaji – na wawili kati yao wamezalisha mabao mengi zaidi ya wachezaji
wengine msimu huu.
Giroud na Ozil
Mabao matano yametengenezwa na
Neymar na kufungwa na Suarez, na mabao megine manne yametengenezwa na Suarez na
kufungwa na Neymar, imeifanya pacha hiyo kuwa bora zaidi ya nyingine za ligi
tano za Ulaya.
Lakini pacha ya Arsenal inayoundwa
na Olivier Giroud na Mesut Ozil haiko mbali kwa kushika nafasi ya pili.
Ozil amemtengenezea Giroud nafasi
sita za kufunga msimu huu, na kumfanya straika huyo wa kimataifa wa Ufaransa
kuisaidia Arsenal kuongoza Ligi Kuu.
Hali kama hiyo imetokea kwa Everton
ambapo, straika Romelu Lukaku amefunga mabao sita kutokana na pasi za Gerard
Deulofeu, hata hivyo, Lukaku hakutoa pasi yoyote ya mwisho kumsaidia Deulofou
kufunga.
Straika
wa zamani wa Tottenham, Roberto Soldado ametoa pasi tano za mwisho kwa, Cedric
Bakambu wakiitumikia Villarreal ya Hispania, huku mwenzake huyo akimtengenezeaa
nafasi moja.
Jamie Vardy na Riyad Mahrez wa Leicester wanashika nafasi ya sita. Mahrez akitoa pasi za mwisho nne kwa Vardy, na Vardy akimtengenezea
mwenzake mabao mawili.
Kati ya wote waliotengeneza mabao
sita au zaidi, Pacha sita kati ya 13 zinatoka katika Ligi Kuu England.
Mahrez na Vardy
Uwepo wa viungo tu hauwezi kusidia
ipasavyo uwezo wa washambuliaji wawili, kama ilivyo kwa Watford, hiyo ni moja
vitu vinavyotengeneza nguzo muhimu, huku uwepo wa viungo wabunifu ukibaki kuwa
imara.
Labda kwa mshangao, ushiriki
mwingine mzuri wa Leicester ukiongeza orodha ya uwepo wa Mahrez na Mark Albrighton,
huku mchezaji huyo wa zamani wa Aston Villa akiwa na pasi za mwisho tano kwa
mwenzake.
Deeny na Ighalo
Ushindi mkubwa wa Everton wa mabao
6-2 dhidi ya Sunderland November mwaka jana ulionyesha mwanga kwa, pia, ushindi
huo ukiibua maswali kwa washambuliaji Arouna Kone na Lukaku. Walifunga mabao manne wenyewe katika ushindi
huo.
Post a Comment