Rooney
MANCHESTER,
ENGLAND
WAYNE
ROONEY amewaambia mashabiki wa Manchester United hawafanyi vizuri wanavyomtupia
lawama kocha, Louis van Gaal kwa matatizo yanayotokea katika klabu hiyo msimu
huu.
Straika
huyo mwenye umri wa miaka 30 amekiri wachezaji
wa Man United wamekuwa tatizo la kufanya vibaya na siyo kocha.
Kocha
Van Gaal hatajiuzulu lakini anakubali kupatwa na msukosuko katika kuifundisha
klabu hiyo. Tatizo lake ni sawa na kupigwa na wimbi.
Kocha Van Gaal akiwa na benchi lake la ufundi
Kocha
huyo alizomewa na mashabiki wa uwanja wa nyumbani wa Old Trafford wiki
iliyopita baada ya kufungwa na Southampton bao 1-0.
Ijumaa
usiku katika mchezo wa Kombe la FA, United iliifunga Derby County na kufanya kocha huyo kuwa katika auheni ya
muda mfupi.
Rooney na Van Gaal
Kocha
Van Gaali ameweka historia mbaya United mpaka kufikia sasa katika msimamo wa
Ligi Kuu msimu huu na kujiweka mara kwa mara katika wakati mgumu kutokana na
ufundishaji wake kupondwa na mashabiki wake.
Hata
hivyo, Rooney amewataka wachezaji wenzake kuwajibika kwa kutolewa mapema kwenye
Ligi ya Mabingwa Ulaya na kujituma ili kuweza kufuzu kwa mashindano hayo msimu
ujao.
“Sisi ndio tunakuwa uwanjani, kwa hiyo
wachezaji tunatakiwa kuwa na majukumu kwa kiwango cha uchezaji na matokeo.
“Tunapaswa
kusimama imara na kukubali lawama zinapotokea. Tunahitaji kushinda, kwa hakika
tunahitaji ushindi — na tumejaribu. Hata ukijotoa kwa asilimia 100, haitoshi,”
alisema kapteni huyo wa Man United.
Rooney,
alifunga bao la kwanza katika ushindi wa
mabao 3-1 dhidi ya Derby, amekiri tuhuma kwamba Van Gaal hajatekeza kwa kiwango
cha kutosha timu hiyo kucheza soka la
kuvutia.
“Kocha
ametupa uhuru wa kutosha katika uchezaji na nadhani unaweza kuona tofauti
katika timu,” alisema.
‘Unaweza
kuona tulifurahia mchezo, tumefunga baadhi ya mabao mazuri na kuweza kustahili
kuibuka na ushindi, tunategemea tunategemea kuwa katika kiwango kama hicho
dhidi ya Stoke Jumanne.”
Post a Comment