Van Gaal akitafakari
Charles Austin akishangilia bao lake.
Raha ya ushindi....
Wachezaji wa Man United wakiwa wamekata tamaa.
MANCHESTER,
ENGLAND
CHARLIE
Austin aliingia kutokea katika benchi na kuipa ushindi Southampton ‘The Saints’
dhidi ya Manchester United katika dimba la Old Trafford na kuifanya United
kupoteza mchezo wake wa kwanza kati ya mitano.
Kocha
Louis van Gaal anajua kuna uasi ndani ya Manchester United.Kocha huyo wa Old Trafford anaamini kitendo cha mashabiki kuzomea kufuatia kipigo hicho kilikuwa ni kibaya sana katika utawala wake klabuni hapo.
Mashabiki wa United walimzoemea Mholanzi huyo baada ya usajili mpya wa Southampton, Charlie Austin kufunga bao la kichwa katika dakika ya 87 uwanjani Old Trafford.
Van Gaal alisema: “Ndio kilikuwa kitendo kibaya. Kwa sababu kilikuwa ni kitendo cha wazi, na naweza kuamini hivyo kwa sababu nimeshuhudia mechi mbaya.
“Huwezi kusema kuwa mashabiki hawako sawa. Wako sawa na wamekatishwa tamaa na wana haki ya kunizomea. Lakini ilitakiwa tuwe pamoja katika kipindi hiki ambacho tuna majeruhi wengi.
“Kilikuwa kiwango kibovu kwa sababu soka siyo kujilinda tu lakini pia kutengeneza nafasi na hatukutengeneza nafasi.
“Wapinzani wetu walistahili kwa hiyo ulikuwa mchezo mbaya kwa mashabiki. Tulijitahidi kutengeneza nafasi kwa sababu wapinzani wetu walijipanga na walikuwa na mabeki watano na walikuwa wagumu lakini tulitakiwa kutengeneza nafasi zaidi tulivyofanya.”
Bosi huyo mwenye umri wa miaka 64 ameweka wazi kuwa kunahitajika mabadiliko kwa kwa baadhi ya nyota wake ambao walipoteza kasi baada ya mchezo wa ushindi wa1-0 dhidi ya Liverpool wiki iliyopita na ule wa Swansea kwenye ligi na dhidi ya Sheffield United kwenye Kombe la FA.
Van Gaal aliendelea: “ Tumepoteza kasi yetu baada ya baadhi ya mafanikio ya mwaka 2016 na inatia huruma.
“Siwezi kubadilkisha mawazo ya mashabiki. Ninaweza kufanya kazi kwa bidii na wachezaji wangu kurudisha kiwango na ndicho ninachokifanya.
“Kwa kweli nimekata tamaa na nafahamu hilo lakini natakiwa kufikiriab na tayari nimeshaanza kujiuliza ninawezaje kubadilisha hilo, kwa sababu tunatakiwa kubadilisha hali hii. Hiyo ni kazi yangu na siyo kazi rahisi kwa muda huu.”
Van Gaal alikiri uamuzi wake wa kumtoa Marouane Fellaini na kumwingiza Juan Mata wakati wa mapumziko kimeifanya United kuwa katika mazingiza magumu na kukatika katikati, hasa baada ya beki, Matteo Darmian alipokimbizwa hospitalibaada ya kugongana na Shane Long.
Post a Comment