0
Mourinho na Giggs wanaoigawa bodi ya United.
Guardiola ametajwa kutakiwa Man United kwa mara ya pili.
MANCHESTER, ENGLAND
MANCHESTER UNITED imegawanyika pande mbili kuhusiana na kocha yupi anayefaa kuichukua nafasi ya Louis van Gaal.
Ndani ya Bodi ya Man United kuna baadhi wanamsapoti klocha msaidizi, Ryan Giggs apewe timu na kundi lingine la bodi hiyo linamtaka kocha wa zamani wa Chelsea, Jose Mourinho.
Lakini Mtendaji Mkuu wa Man United, Ed Woodward ambaye  pia ni mwenyekiti – bado anadhani Louis van Gaal anaweza kumaliza kwa kishindo.
Hiyo inaweza kumfanya Van Gaal, 64, kuendelea kukinoa kikosi hicho kwa msimu mwingine, wakati anaingia katika mwaka wa mwisho wa mkataba wake.
Hatimaye, wamiliki wa Man United, Wamarekani familia ya Glazer ndio pekee watakaokuwa na uamuzi wa mwisho juu ya suala hilo.
Kocha msaidizi na mkongwe kwa klabu hiyo Giggs, 42, amekuwa akionekana kuandaliwa tangu mapema kuchukua mikoba hiyo ya Old Trafford.
Lakini mtu mmoja mwenye sauti ndani ya klabu anaamini Mourinho, ambaye Jumanne atatimiza miaka 53, anapaswa kupewa nafasi ya kuiongoza klabu hiyo kutokana na rekodi yake ya kushinda mataji.
Kocha Pep Guardiola alihusishwa kuhamia United kwa mara nyingine wiki iliyopita kuna madai kwamba anapenda kuitumukia klabu hiyo kuliko Manchester City.
Lakini katika mahitaji yake Mhispania, 45, atakayeachia ngazi Bayern Munich mwishoni mwa msimu, yuko makini kuhusu suala la usajili na anafahamu  United haiwezi kutimiza mahitaji yake katika suala hilo.
Mpaka sasa, Manchester City ina uhakika wa kupata huduma za kocha huyo wa zamani wa Barcelona.
Hata Chelsea ingependa kumchukua Guardiola mwishoni mwa msimu, lakini imekata tamaa baada ya kushindwa kumchukua mara mbili miaka mitano iliyopita.
 Guardiola anapenda kukaa London, Arsenal ingekuwa ni chaguo lake la kwanza lakini alibaini kuwa nafasi ya Arsene Wenger kuachia ngazi ni finyu mno.
Yote hayo yanaiacha Man City kuwa timu pekee ya kumchukua Guardiola kwa sababu ya uwepo wa kina Ferran Soriano na Txiki Begiristain aliowahi kufanya nao kazi Barcelona.
 


Post a Comment

 
Top