0
Liverpool wakishangilia
 Lallana baada ya kufunga bao la tano
  • NOWRICH, ENGLAND
  • LIVERPOOL imepata ushindi wa maajabu ugenini dhidi ya Nowrich City baada ya straika Adam Lallana kufunga bao la dakika za mwisho wakati mashabiki wakiamini mchezo huo ungeisha kwa sare ya mabao 4-4. Norwich City ilisawazisha bao bao la Roberto Firmino katika dakika ya 29 kupitia kwa Mbokani Bezua. Dakika 41, Naismith wa Norwich City aliipatia timu yake bao la pili. Kama haitoshi, Hoolahan wa Nowrich aliipatia timu yake bao la tatu kwa mkwaju wa penalti. Wakati mashabiki wa Liverpool wakianza kukata tamaa, kiungo wao Henderson alisawazisha kwa penalty na kuyafanya matokeo kuwa 3-2.

Dakika ya 63,Roberto Firmono akaipatia tena Liverpool bao la kusawazisha na kufanya matokeo kuwa 3-3.
Milner aliipa Liverpool bao la nne katika dakika ya 75 na kuifanya timu hiyo kuamini kuwa itaibuka na ushindi.
Lakini Bassong wa Nowrich alipigilia msumari na kuamini timu yake imesawazisha bao hilo na kuambulia pointi moja bada ya kufunga katika dakika ya pili ya nyongeza baada ya dakika 90. (90'+2).
Baadhi yamashabiki walishaanda kutoka uwanjani ndipo Lallana alipofunga bao la tano katika dakika ya tano ya nyongeza (90'+5) na kuipa timu yake pointi tatu.
 

Post a Comment

 
Top