Giroud akifurahi baada ya kufunga bao.
Giroud akijuta baada ya kukosa bao
Giroud
LONDON, ENGLAND
OLIVER Giroud ni mfungaji bora katika
klabu ya Arsenal inayoongoza Ligi Kuu England ikiwa kwenye mbio za kusaka
ubingwa, lakini baadhi ya mashabiki wa timu yake hawampi heshima anayostahili.
Giroud anataka kukumbukwa kama
mpchachika mabao muungwana.
Straika
huyo anajua kama mashabiki wa Arsenal wamegawanyika juu yake na anakubali na
kudai kuwa kila siku wenye chuki hawakosekani.Lakini Mfaransa huyo amejipangia lengo la kufunga mabao 30 ambayo anaamini yatawanyamazisha wale wenye shaka naye na kuisaidia Arsenal kushinda taji la Ligi Kuu.
Alipoulizwa kama anajisikia kushushwa thamani, Giroud alisema: “Sijiulizi kuhusu hilo. Najaribu kufanya kila kitu kwa ubora kuisaidia timu yangu. Nataka kujitoa kwa kila kitu na kuongeza juhudi kila siku.
“Hilo nimelifanya mwaka huu na ninategemea nitafikia malengo yangu, idadi yangu ya mabao na kuifanya timu yangu itwae taji la Ligi Kuu England. Hilo ni jambo kubwa sana kwangu.
“Kila siku utakutana na wenye chuki na watu wasiokupenda, lakini hilo siyo kitu kwangu. Sitapoteza usingizi wala kufanya kitu kama hicho.”
Giroud amesajiliwa kutoka Montpellier mwaka 2012 kwa Pauni 13 milioni, anacheza kama straika wa kizamani wa Kiingereza.
Na hilo linadaiwa ndio sababu ya baadhi ya mashabiki wa Arsenal kudhani kwamba wanahitaji straika mwingine wa gharama na mwenye jina kubwa katika soka.
Lakini Giroud yuko kamili msimu huu na tayari kupambana na John Terry katika Uwanja wa Emirates Jumapili hii.
Post a Comment