0
Kocha wa Southampton, Koeman
 Koeman akiwa kazini
 Koeman
 Kocha wa muda wa Chelsea, Guus Hiddink


SOUTHAMPTON,ENGLAND
RONALD KOEMAN anayeinoa Southampton amemtaka kocha wa muda wa Chelsea, Guus Hiddink kulipendekeza jina lake kwa bilionea Roman Abramovich ili amepewe nafasi ya kuinoa Chelsea mwishoni mwa msimu.
Hata hivyo, Koeman atakutana na wakati mgumu kupata kibarua hicho kutoka kwa kocha, Massimiliano Allegri anayedaiwa kutaka kupewa nafasi hiyo.
Mdachi huyo mwenye umri wa miaka, 52, ametoa neno kwa Mdachi mwenzake, Hiddink kwamba ampigie chapuo ili aipate nafasi hiyo kwani akiipata atafanya maajabu Chelsea.
Koeman aliimbia Radio ya Uholanzi: “Kama Guus atasema maneno mazuri juu yangu, huo utakuwa ushawishi mkubwa sana.”
Hiddink ndiye bosi wa Chelsea wa muda atakayeitumikia timu hiyo hadi mwishoni mwa msimu.  Ameshika nafasi hiyo kwa mara ya pili, kutoka kwa Jose Mourinho aliyefukuzwa mwezi uliopita.
 Koeman, ambaye alishatwaa mataji akiwa anafundisha Uholanzi akiwa na klabu za Ajax, Feyenoord na PSV Eindhoven, anatamani kupata nafasi ya kuinoa klabu kubwa.
Aliongeza: “Kwa uhakika kitu hicho huwa kinakuwa katika akili yangu mara kwa mara.
“Kila siku nataka kupata mafanikio ya kiwango cha juu. Hilo tayari limeshatokea Uholanzi na nataka sana kupata mafaniko nje ya nchi.”
Koeman alifanikiwa kuchukua mikoba ya kocha wa Tottenham, Mauricio Pochettino Juni 2014 baada ya Muargentina huyo kuondoka.
Na bosi huyo wa zamani wa Valencia ameingoza Southampton kumaliza katika nafasi ya saba ya Ligi Kuu, pamoja na baadhi ya klabu kuchukua wachezaji wake mahiri mwishoni mwa msimu uliopita.

Post a Comment

 
Top