Ronaldo na Neymar picha ndogo Ronaldo akiwa Morocco na rafiki yake
Ronaldo
Neymar
MADRID, HISPANIA
HAYAWI hawayi hatimaye yamekuwa, habari kutoka
Hispania zinasema nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo amepigwa marufuku kufanya
safari za kwenda Morocco na Rais wa Real Madrid, Florentino Perez.
Supastaa
huyo wa Ureno, 31, amekuwa akifanya ziara za kumtembelea rafiki yake bondia wa
mchezo wa ‘kickboxer’ Badr Hari, anayedaiwa kuingia naye katika uhusiano wa
kishogaNa rais huyo wa Bernabeu amegundua kuwa safari hizo zimemwathiri Ronaldo na kumfanya ashuke kiwango.
Ronaldo amekuwa akitumia ndege yake binafsi yenye thamani ya Pauni14 milioni kwenda Kaskazini mwa Afrika baada ya mazoezi ya asubuhi, na kurudi jioni.
Kwa mujibu wa Gazeti la El Espanol, nyota huyo wa zamani wa Manchester United amekuwa akifanya safari zake kila Jumatatu hadi Alhamisi na Perez ameona sasa inatosha.
Rais Perez amepinga tabia hiyo ya Ronaldo na kusimamisha kuhesabiwa safari za staa huyo na rafiki yake Mfalme wa Morocco, Mohamed VI, kila anapoingia katika nchi hiyo.
Mapema wiki iliyopita Real Madrid ilikuwa ikimpigia hesabu staa wa Barcelona, Neymar kutokana na safari hizo za Ronaldo.
Na hata kufukuzwa kwa kocha, Rafa Benitez na nafasi yake kuchukuliwa na Zinedine Zidane, Bernabeu kulitakiwa kwenda sambamba na kufunguliwa mlango kwa Ronaldo kama mpango wa kumnasa Neymar ungekuwa unaenda sawa.
Post a Comment