0
Guardiola
 Mourinho
 Van Gaal
NA PRIVA ABIUD

UGONJWA wa Jose Mourinho ni kupata mafanikio ya muda mfupi, lakini mambo yanapokwenda kombo huanza kuwasakama watu wanaomzunguka. 
Atawaonyeshea vidole ovyo na ufalme wake utaanza kuporomoka ghafla. Kingine ataanza kuwanyanyasa wachezaji wadogo.
Turudi nyuma kidogo. Watu wengi wanajiuliza kwa nini inasemekana ulikuwepo ugomvi kati ya Pep Guardiola na marehemu Tito Vilanova? Najua inakatazwa kumsema vibaya marehemu, ila hapa sitamsema vibaya Vilanova.
 Wakati ule Vilanova alipokuwa akifanya kazi na Guardiola pale Barcelona walikubaliana kuwa watasitisha vibarua vyao na kutimkia Manchester United.
Lakini mara baada ya Guardiola kutangaza kung'oka Barcelona kesho yake alishangazwa na taarifa kuwa aliyekuwa kocha wake msaidizi, Vilanova ametajwa kuwa kocha mkuu wa Barcalena!
Guardiola alikereka sana na kitendo kile, hakuwa na namna na baadaye alielekea Marekani kula bata. Huku nyuma Vilanova aliugua na pamoja na ugomvi wao, alienda kumuona  hospitali.
Wakati ule Sir Alex Ferguson alifanya mikutano zaidi ya 12 na Guardiola kule Marekani akimsihi ajiunge na United.
Hata hivyo, Ferguson alizubaa mwishowe Guardiola alijiunga Bayern Munich.  Tageti ya mwisho ya Fergie kupata mrithi wake alikuwa ni Mourinho.
Abramovich umekula maharage ya wapi?
Mwaka  2007 Mourinho alimalizana na Chelsea lakini makubaliano yao ni kwamba asirudi kufundisha timu yoyote ya England kwa wakati ule. Mwaka 2015 Mourinho amemalizana na Chelsea lakini mkataba wake haumbani kufundisha klabu yoyote ya Ligi Kuu England.
Hapa napenda nimzungumzie Abramovic ambaye amesahau kuwa Man United na Manchester City zina njaa ya makocha.
Amesahau kuwa Arsene Wenger kichwa chake kinawaka moto kama anaweza akatwaa ubingwa msimu huu. Amesahau kuwa Guardiola amevunja mkataba na Bayern Munich na yupo njiani kwenda England na anajifanya hajui kama Brenden Rodgers amempisha Jurgen Klopp pale Liverpool?

Nani kamloga Abromovich? 
Kwa nini nasema Abramovic amejisahau, nawaza tu, hivi Mourinho akienda United, halafu Guardiola anakwenda Man City! Maana yake nini? kwa vyovyote vile Chelsea itakuwa Underdog (yaani tunasema lazima ipoteze pambano). Kwa sababu tangu mwaka 2002, Mourinho amefundisha timu tano tofauti na kote amebeba ubingwa wa ligi, na kote alitawala na kubadili upepo wa ligi.
Sitaki kumzungumzia sana Guardiola maana hilo lipo wazi, je kama hawa watu wakiwa England nani atakuwa kilaza, kama si Chelsea? Au nawaonea? Ni kocha yupi atapambana na hawa wanaume? Ni kocha yupi atakayeikoa Chelsea midomoni mwa Klopp, Wenger, Guardiola na Mourinho?
Nawasihi kwenye sala za jioni na za asubuhi mkumbuke kuiombea Chelsea.
 Mourinho vs Guardiola
Tuachane na hayo, ninaamini vita itabaki kwa Guardiola na Mourinho, kama Guardiola ataenda Man City.
Hapa  kwa mtazamo tu,ndiye atakayekuwa kilaza. Kutokana na mfumo wake, hauwezi kufanya kazi Ligi Kuu England.
Ligi hiyo inahitaji kasi, nguvu na akili, sio uwezo binafsi wa pasi wala chenga.
Rafiki yangu mmoja aliniuliza je, akibadili na akacheza mpira wa Kiingereza? Mh kwa kiasi fulani Mourinho atapotea. Maana Guardiola ni mastermind (akili nyingi) kwa namna moja. Sikuwa na jibu la moja kwa moja kwa maana sikuwahi kumuona Guardiola na fumo huo. Hivi Guardiola aanategemea acheze mpira wa pasi nyingi pale Britania Stadium?

Mourinho na Man United
 Watu wanasema Mourinho huwa na mafanikio yake ni ya gharama na ya muda mfupi! Swali ni je, kwa gharama walizotumia United wataendelea kumwaga tena pesa? Labda lakini ninachokiona itamchukua muda kubadili mfumo wa Man United kwa sasa!

Guardiola
United inacheza mfumo wa kina Guardiola kwa sasa, Mourinho akija lazima abadilishe, na huko sio kuwavuruga wachezaji?
Bado atataka kuleta wachezaji wake? Lakini usisahau kuwa usajili ni kamari angalia hawa watu, Mohamed Sallah, Juan Cuadrado, André Schürrle, Kevin De Bruyne.
Hapa Mourinho alipoteza, kwa mantiki hiyo atataka kubadili mfumo na kujenga himaya yake. Pili atataka kuleta watu wake ambao mfumo unaweza kuwakataa.
Hivyo, Man United itaingia kwenye kamari ambayo kocha wa zamani wa United, Ron Atkinson na mchezaji wa zamani wa timu hiyo, Bobby Chalton wanamkataa Mourinho na kumtaka Guardiola ambaye hatabadili mfumo ila ataongeza ujuzi wake tu.

Mourinho
Najua Fergie anachanganyikiwa maana anafahamu Guardiola ni mpita njia, na anajua wazi kuwa Bodi ya Man United haimtaki Mourinho ndio karata inayomweka Louis Van Gaal mjini Manchester hadi leo hii. Sijui mwisho wa hii filamu ila kilio changu ni sala kwa ndugu zangu wa darajani. Okey ngoja nipitie.

 

Post a Comment

 
Top