Mwenyekiti wa Crystal Palace, Steve Parish, Adebayor na Perdew
Adebayor akiwa na jezi ya Palace
Adebayor akiwa Spurs.
LONDON,
ENGLAND
EMMANUEL
ADEBAYOR amerejea Ligi Kuu ya England baada ya kukamilisha usajili wa
kushtukiza akijiunga na Crystal Palace.
Crystal
Palece imethibitisha kumnyakua straika huyo wa zamani wa Tottenham kwa mkataba
utakaodumu hadi mwishoni mwa msimu.
Hata
hivyo, taarifa zinasema dili hilo linaweza kuongezwa muda hadi mwishoni mwa
msimu ujao; kimsingi makubaliano ni ya miezi 18 kukiwa na kipengele cha kuweza
kuvunjwa kwa mkataba mwishoni mwa msimu.
Palace
itamlipa Adebayor kiasi cha Pauni 70,000 kwa wiki; huku Spurs akifidia
kiasi kilichobaki cha Pauni 30,000 kwa wiki kutokana na mkataba
alioingia Hart Lane ambao unakwisha Juni.
Akiwa Manchester City
Adebayor
aliondoka Spurs kwa kuridhiana mwezi Septemba; lakini klabu hiyo ya Kaskazini
mwa London bado inawajibika kumlipa mshahara wa Pauni100,000 kwa wiki. Straika huyo mwenye umri wa miaka 31 atavaa
jezi namba 25 akiwa Selhurst Park.
Kusajiliwa
kwa Adebayor kumekuja wakati mwafaka kwa bosi wa klabu hiyo, Alan Perdew
kufuatia kufungiwa mechi tatu na FA kwa straika wake namba moja, Connor Wickham
kwa kufanya fujo na kumuumiza jichoni beki wa Spurs Jan Vertonghen Jumamosi.
Akiwa Arsenal
Mwenyekiti
wa Palace, Steve Parish alitumia Mtandao wa Instagram kumkaribisha Adebayor
akiwa ametuma picha aliyopiga na straika huyo pamoja na kocha Pardew.
Nyota
huyo mkali wa Palace anatarajiwa kuisadia timu hiyo ambayo imeshindwa kupata
ushindi katika michezo sita.
Adebayor
amefunga mabao 18 katika micheezo 59
wakati akiitumikia Spurs lakini aliachwa katika usajili wa kikosi cha wachezaji
25 cha kocha Mauricio Pochettinoc katika Ligi Kuu.
Staa
huyo wa kimataifa wa Togo hakuweza kujiunga na klabu nyingine hadi dirisha la Januari
kwa kuwa alikuwa akifahamika kuwa bado ni
mchezaji halali wa Tottenham.
Ndani ya Spurs
Pia,
alishindwa kukubaliana na uongozi wa Spurs baada ya kukataa kuondoka klabuni
kwa kushindwa kumlipa Pauni 5 milioni iliyobaki katika mkataba wake.
Kabla
ya kujiunga na Palace, Adebayor alidaiwa kutaka kujiunga na kocha wake wa
zamani Tim Sherwood wakati akiwa Villa lakini pande hizo mbili zilishindwa
kuafikiana.
Kwa
mara ya kwanza, Adebayor alisajiliwa katika Ligi Kuu England na Arsenal akitokea
Metz ya Ufaransa kabla ya kwenda
Manchester City kwa Pauni 25 milioni.
Bao
maarufu la straika huyo alilifunga dhidi ya Arsenal uwanjani Etihad na kukimbia
umbali mrefu kwenda kushangilia kwa mashabiki wa timu pinzani waliokuwa na
hasira dhidi yake kwa kumzoemea na kumtolea maneno yenye hasira.
Baadaye
alipelekwa kwa mkopo kwenda Real Madrid mwaka 2011, ambako alifunga mabao
matano katika michezo 14.
Alitolewa
tena kwa mkopo kwenda Tottenham, ambako alimvutia kocha Andre Villas-Boas aliyeamua
kumpa usajili wa kudumu.
Akiwa Madrid
Lakini
kufukuzwa kwa Villas-Boas, Spurs kulimfanya straika huyo kulazimishwa kwenda
kufanya mazoezi na kikosi cha timu hiyo
cha chini ya miaka 21 kabla ya Tim Sherwood kumrudisha kwenye timu ya
wakubwa.
Hata
hivyo, ujio wa kocha Pochettino, White Hart Lane siku za Adebayor zilikuwa
zikihesabika kabla ya kuachwa Septemba
2015.
Post a Comment