1
Mourinho
 Mourinho na Giggs
LONDON, ENGLAND

JOSE Mourinho anadaiwa kuandika barua ya kuomba kazi Manchester United ikiwa na kurasa sita. 

Kwa mujibu wa Gazeti la Independent Mourinho ameandika barua hiyo kuomba kazi Manchester United huku akieleza namna atakavyoweza kuipa klabu hiy mafanikio. Katika barua hiyo, Mourinho pi ameandika  kiu yake ya muda mrefu ya kuifundisha United. Kocha huyo wa zamani wa Real Madrid, Inter Milan na Chelsea amekuwa hana kazi tangu alipotimuliwa na bilionea Roman Abramovich, Desemba kufuatia mambo kwenda mrama Chelsea msimu huu.

 Katika  barua hiyo Mourinho aliandika kwamba atachukua uamuzi mgumu ili kuirudisha United katika mafanikio yake ambayo mpaka sasa haijashinda taji lolote tangu alipostaafu Sir Alex Ferguson mwaka 2013.
Manchester United inashika nafasi ya tano katika msimamo wa Ligi Kuu baada ya kichapo cha Jumamosi  cha bao 1-0 kutokwa kwa Southampton.
Kumekuwepo ongezeko la kutoaminika kwa kocha Van Gaal, Old Trafford baada ya kuzomewa na mashabiki mara baada ya kumalizaka kwa mchezo huo.
Awali ilidhaniwa kuwa Mholanzi huyo angeondoka  katika mechi za vipigo vinne vya mwezi Desemba,  lakini ushindi mara tatu na sare mbili  katika mashindano yote tangu Sikukuuya Boxing Day na pamoja na kupoteza kwa Stoke Van Gaala aliendelea na kibarua chake.
Mourinho amekuwa mstari wa mbele katika harakati za kurithi mikoba ya Van Gaal kama kocha huyo atajiuzulu au kufukuzwa.
Hata hivyo, kuna tetesi kwamba kuna kundi la wanabodi wa Manchester United hawamtaki kocha huyo na wanaamini nafasi hiyo inaweza kuzibwa na kocha msaidizi, Ryan Giggs ambaye ni mchezaji wa muda mrefu wa klabu hiyo.
Kundi lingine la wanabodi linaamini Mourinho ndiye anayefaa kuchukua nafasi hiyo Old Trafford kutokana na uzoefu wake wa kutwaa mataji.
Hata hivyo, wakala wa Mourinho, Jorge Mendes, ambaye pia ni wakala wa Cristiano Ronaldo, James Rodriguez na Angel Di Maria amekanusha tuhuma hizo.
 " Haijawahi kutokea  kwa yeyote  mwenye hadhi ya kama ya Mourinho kuandika barua  katika klabu kuomba kazi.
"Kwa hakika hii ni dharau na moja kwa moja inasikitisha," alisema Mendes.
 

Post a Comment

  1. Nimeipenda sana ni habari nzuri sana, endeleeni kutupa habari za kina tafadhali

    ReplyDelete

 
Top